Pancake yenye honey-orange syrup na matunda

Pancakes ni rahisi kuandaa na hazichukui muda sana. Unaweza kula cha chai au kinywaji chochote na ukafurahi.

Mahitaji

 • Unga vikombe 3
 • Sukari nyeupe vijiko 2 vya chakula
 • Baking powder vijiko 3 vya chai
 • Baking soda kijiko 1 cha chai
 • Chumvi nusu kijiko cha chai
 • Butter milk vikombe 2
 • Maziwa kikombe 1
 • Mayai 3
 • Butter nusu kikombe
 • Mdalasini nusu kijiko cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Chukua bakuli, weka unga, sukari, baking powder, baking soda, mdalasini na chumvi.
 • Yeyusha butter, chukua bakuli lingine weka butrermilk, maziwa, butter na mayai.
 • Koroga mchanganyiko huo weka pembeni. Usichanganye na unga kwanza mpaka utakapo anza kupika.
 • Chukua mchanganyiko wenye maziwa, mimina kwenye mchanganyiko wenye unga. Sasa changanya vizuri hakikisha hauwi mzito sana wala mwepesi sana.
 • Weka frying pan kwenye moto, ambayo vitu havishiki chini ukiitumia (non stick pan).
 • Chota mchanganyiko huo, weka upawa mmoja kwenye pan, moto uwe mdogo na ukiona imeanza kutoa vitundu geuza upande mwingine.
 • Hakikisha pancakes zinakua rangi ya kahawia. Fata utaratibu huo huo kwa mchanganyiko wote hadi uishe.
 • Ukipenda weka butter au syrup yoyote mimi nimetumia ya asali na machungwa. Nikaweka na matunda. Jirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Tambi zenye iliki na sukari
dakika 8
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.