Peanut butter cookies

Cookies ni chakula kizuri kinachopendwa na watu wengi hasa watoto. Unaweza kula cookies na familia na mkafurahi. Kula wakati wowote na kinywaji chochote.

Mahitaji

 • Unga vikombe 2 na nusu
 • Butter (isiyo na chumvi) kikombe 1
 • Peanut butter kikombe 1
 • Sukari nyeupe kikombe 1
 • Sukari ya brown kikombe 1
 • Vanila nusu kijiko cha chai
 • Mayai 2
 • Baking powder kijiko 1 cha chai
 • Baking soda robo tatu ya kijiko cha chai
 • Chumvi nusu kijiko cha chai
 • Karanga (zilizokaangwa ziponde na kitu zivunjike vunjike)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Chukua bakuli kubwa au sufuria. Weka butter, sukari nyeupe, sukari ya brown, peanut butter na yai. Changanya kwa muda mpaka sukari ilainike.
 • Chukua sufuria lingine au bakuli, weka unga, baking powder, baking soda na chumvi pamoja. 
 • Uchekeche kisha uweke kwenye mchanganyiko wenye butter, koroga vizuri uchanganyikane.
 • Ukiona upo tayari, chukua karanga zilizokaangwa zikapondwa umwagie kwenye mchanganyiko wako na vanila. Koroga.
 • Weka kwenye jokofu kwa nusu saa. 
 • Toa anza kutengeneza shape unazotaka. Chombo utakacho okea cookies  kipake butter.
 • Panga cookies kwenye pan kisha,Ziweke kwenye oven vioke ndani ya dakika 9 hadi 10.
 • Ziepua ziache zipoe kwa dakika tano. Anza kujiramba.

MAPISHI YAPENDWAYO

Beef masala
dakika 30
Walaji: 4

Supu ya ulimi wa ng'ombe
dakika 40
Walaji: 1

Kuku wa kukaanga wa ndimu
dakika 10
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.