Pilau la basmati

Mchele wa basmati unatoa matokeo mazuri sana kwenye kupikia. Pilau hili la nyama kwa mchele wa basmati linakupa matokeo mazuri. Chakula hiki ni kizuri kupika kwa familia nzima, hasa kwenye mlo wa pamoja.

Mahitaji

 • Njegere ¼ kilo
 • Mchele wa basmati kilo 1
 • Nyama kilo 1, chemsha vizuri hadi iive
 • Kitunguu saumu 1 kikubwa, menya na twanga
 • Vitunguu maji 5, kata umbo la duara
 • Mdalasini kijiko 1 kikubwa
 • Bizari nyembamba  ½ kijiko kidogo
 • Karoti 2, kata vipande vidogo
 • Viungo vya pilau, unavyopendelea
 • Supu ya nyama ya moto
 • Chumvi kijiko 1 kidogo

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kutumia viungo vya pilau unavyopendelea ili kukipa chakula ladha bora zaidi.

 • Bandika sufuria jikoni, weka mafuta ya kula. Mafuta yakipata moto weka nyama kisha kaanga hadi ianze kubadilika rangi na kuwa kahawia. Weka vitunguu maji, pika hadi vibadilike rangi. Weka kitunguu saumu, pika kwa dakika 3 hadi 5 huku ukikoroga mara kwa mara.
 • Weka njegere na viungo vilivyobaki kwenye sufuria, kasoro karoti na chumvi. Koroga  mpaka viungo vianze kutoa harufu nzuri kisha weka mchele. Kaanga mchele kwa dakika 20 kwenye moto mdogo kisha weka chumvi. Koroga chakula pamoja kisha weka supu kiasi.
 • Supu ikikauka punguza moto, au mkaa, ili uwe na moto wa wastani. Weka karoti, koroga ili karoti zichanganyikane na chakula. Funika na acha chakula kiive taratibu kwa mvuke. Baada ya dakika 15, funua na geuza chakula.
 • Chakula kitakuwa tayari kimeiva, andaa na ujirambe.

pilau-basmati-misosi-poor


MAPISHI YAPENDWAYO

Uji wa mchele na ndizi
dakika 35
Walaji: 1

Creamy garlic potato
dakika 40
Walaji: 1

Chicken curry
dakika 30
Walaji: 5

Butter chicken
dakika 45
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.