Pilipili

Pilipili ni kiungo kinachompa mlaji hamu ya kula chakula,pilipili inaeza kuekwa kwenye chakula chochote mlaji atakapopenda na kufanya mlaji apende chakula chake.

Mahitaji

 • Carrots 3 kubwa
 • Pilipili hoho 1
 • Vitunguu saumu 3
 • Vitunguu maji 5
 • Tangawizi 1
 • Majani ya giligiliani
 • Ndimu
 • Chumvi
 • Mafuta kidogo sana
 • Pilipili mbuzi 3 au utakavyopenda
 • Nyanya 3 zilizoiva vizuri
 • Pilipili ya unga vijiko 2 vikubwa vya chakula
 • Oyster sauce kikombe 1 cha kahawa

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Menya nyanya,hoho,carrots,vitunguu maji,vitunguu saumu,tangawizi,majani ya giligilian yachambue.
 • Kata kata vitunguu maji na nyanya weka bakuli tofauti,twanga vitunguu saumu na majani ya giligiliani,kwangua carrots pia katakata pilipili hoho.
 • Bandika mafuta jikono yakipata moto weka vitunguu maji koroga dakika 2 weka vitunguu saumu na giligiliani koroga tia tangawizi kisha hoho na carrots.
 • Acha kidogo weka nyanya kisha weka pilipili ya unga kamulia ndimu tia chumvi funika mpaka nyanya iive vizuri katia pilipili zako dakika tano baada ya kueka pilipili weka oyster sauce acha ichemke kisha epua iache ipoe.
 • Ukiona imepoa ieke kwenye blender isage hapo pilipili yako itakua tayari kwa kujiramba.
 • Nahakika utaipenda sana.

MAPISHI YAPENDWAYO

Bagia za dengu
dakika 20
Walaji: 4

Tambi za maziwa na cheese
dakika 10
Walaji: 2

Biscuits za raspberry
dakika 15
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.