Pilipili ya maembe ya kusaga

Pilipili ni nzuri sana mana humpa mtu hamu ya kula chakula na akakifurahia.

Mahitaji

 • Embe bichi lililokomaa 1
  Karoti 2
  Vitunguu maji 2 vikubwa
  Vitunguu saumu 2
  Tangawizi kubwa 1
  Pilipili manga vijiko 3 vya chakula
  Nyanya 2 kubwa
  Pilipili mbuzi 3
  Vineger vijiko 3 vya chakula
  Chumvi
  Mbegu za cumin kijiko 1
  Binzari kijiko 1
  Limao 1
  Curry powder
  Maji

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Menya embe, karoti, kitunguu maji, tangawizi, nyanya na kitunguu saumu vikate kate.
  Twanga kitunguu saumu na tangawizi.
  Chukua sufuria, weka embe, karoti, vitunguu maji, vitunguu saumu, tangawizi, pilipili manga, nyanya, pilipili mbuzi, vineger, kisha ongeza maji na chumvi alafu bandika jikoni.
  Acha ichemke mpaka maji yaanze kuisha ibaki rojo.
  Weka mbegu za cumin, binzari, curry powder kamulia na ndimu. Ongeza maji kikombe kimoja cha kahawa alafu funika na punguza moto.
  Baada ya dakika kumi epua, iache pembeni ipoe kisha saga.

MAPISHI YAPENDWAYO

Chips mayai na mboga za majani
dakika 20
Walaji: 2

Mishikaki ya kupaka
dakika 30
Walaji: 4

Ugali wa muhogo na mlenda
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.