Pizza Margherita ya kutengeneza nyumbani

Siri kubwa ya kutengeneza pizza nzuri ni kutumia viungo vizuri na bora kwa vipimo sahihi. Mapishi haya ni mazuri kwa mlo wa familia, chakula bora chenye virutubisho. Ni chakula kizuri kwa mlo mwepesi wa jioni.

Mahitaji

Kwa ajili ya unga:

 • Vijiko 2 vya chai vya hamira (yeast)
 • Vikombe 1 ¾ vya unga wa ngano. Tenganisha, weka kidogo pembeni
 • ¾ ya kikombe cha maji ya uvuguvugu
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • ½ kijiko cha mafuta ya Olive (Mafuta ya mizeituni)

Kwa ajili ya pizza topping:

 • Kopo 1 la nyanya za kusaga (Nyanya 3 - 5)
 • Vitunguu saumu 2 vilivyosagwa
 • Vijiko vikubwa 2 vya olive oil
 • Sukari ¼ kijiko cha chai
 • Gramu 100 za jibini ya mozzarella (cheese) iliyokatwa vipande vyembamba
 • Sausage au kiambato chochote ambacho ungependelea kuweka kwenye pizza. (Kata vipande vidogo vidogo ili uweze kuweka vizuri juu ya pizza)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Andaa unga

 • Changanya hamira, unga wa ngano kijiko 1 cha chai, ¼ kikombe cha maji ya uvuguvugu kwenye bakuli. Acha itumie hadi yageuke rangi ya maziwa – inachukua kama dakika 5.

Kama mchanganyiko hauweki rangi, mwaga na changanya tena na hamira nyingine.

 • Ongeza vikombe 1¼  vya unga, ½ kikombe cha maji yaliyobaki, chumvi, na mafuta ya kula. Changanya hadi iwe laini.  
 • Kanda unga kwenye sehemu bapa, nyunyizia unga mara kwa mara unga wako unaposhika zaidi, hadi ulainike na uanze kuvutika – takribani dakika 8. Zungusha kwenye umbo la mpira, weka kwenye bakuli au sufuria, nyunyizia unga kwa juu, funika na mfuniko na acha unga uumuke kwa muda – inachukua takribani saa moja na robo.

doughball

Andaa sauce ya nyanya wakati unga unaumuka

 • Weka nyanya kwenye blender ili kuzisaga. Kama hazijasagwa bado.
 • Pika vitunguu saumu na mafuta ya kula kwenye kikaango kwa joto la wastani – takribani dakika 2.
 • Ongeza nyanya zilizosagwa, sukari na 1/8 ya kijiko cha chai. Usifunike, pika mchanganyiko huku ukiwa unakoroga mara kwa mara, hadi mchanganyiko upungue na maji yakauke. Inachukua takribani dakika 40. Epua na acha ipoe.

pizza-sauce

Pasha moto pizza stone na oven wakati unga unaumuka

 • Takribani dakika 45 kabla ya kupika pizza, pasha moto oven kwenye nyuzijoto 250°C. Kama unatumia pizza stone, liweke kwenye ngazi ya chini kabisa ya oven.

Tengeneza unga kwenye umbo la pizza

 • Tenga unga kwenye mabonge madogo yanayofaa kwa pizza. Nyunyiza unga juu yake. Sambaza unga vizuri na mikono, iwe kwenye umbo la mviringo.

Weka pizza Jikoni

 • Sambaza sauce ya nyanya juu ya unga wa pizza, huku ukiacha upana wa nchi 1 toka pembeni.

sauceon2

 • Panga cheese (jibini) juu yake. Weka na vitu vingine unavyopenda (kama umendaa sausage au nyanya mbichi)

minipizzastocook2

 • Weka pizza kwenye pizza stone, ndani ya oven. Acha ikae hadi unga ukauke na ubadilike uwe rangi ya udongo (brown) na jibini (cheese) ziwe rangi ya dhahabu na zinatoa povu. Inachukua takribani dakika 13 hadi 16.

intheovenone

 • Toa pizza toka kwenye oven, weka kwenye ubao wa kukakia. Acha ipoe kwa dakika 5. Kisha unaweza kukata.

TIP: Unga unaweza kuandaliwa na kuacha uumuke usiku mzima kwa kuhifadhiwa kwenye jokofu. Kabla ya kutengeza pizza, uache ukae kwenye joto la kawaida.

Sauce ya nyanya inaweza kutengenezwa siku 5 kabla na kuwekwa pilipili kwa ajili ya ladha.


MAPISHI YAPENDWAYO

Mkate wa kuku na mayai yake
dakika 40
Walaji: 4

Viazi vya mboga mboga
dakika 18
Walaji: 2

Salad ya mahindi na samaki
dakika 0
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.