Pizza yenye sausage topping

Pizza ni chakula kizuri, chepesi na bora kula wakati wowote. Hapa kwenye hii pizza tunaweka sausage juu yake ili kuleta ladha zaidi. Unaweza kutumia sausage zozote upendazo au hata nyama kama unapendezewa zaidi.

Mahitaji

Kwa ajili ya unga:

 • Vijiko 2 vya chai vya hamira (yeast)
 • Vikombe 1 ¾ vya unga wa ngano. Tenganisha, weka kidogo pembeni
 • ¾ ya kikombe cha maji ya uvuguvugu
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • ½ kijiko cha mafuta ya Olive (Mafuta ya mizeituni)

Kwa ajili ya pizza topping:

 • Kopo 1 la nyanya za kusaga (Nyanya 3 - 5)
 • Vitunguu saumu 2 vilivyosagwa
 • Vijiko vikubwa 2 vya olive oil
 • Sukari ¼ kijiko cha chai
 • Gramu 100 za jibini ya mozzarella (cheese) iliyokatwa vipande vyembamba
 • Sausage au kiambato chochote ambacho ungependelea kuweka kwenye pizza. (Kata vipande vidogo vidogo ili uweze kuweka vizuri juu ya pizza)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Tunaandaa pizza ya sausage ambayo ikishaiva itakuwa inaonekana kama hivi:

pizza-5

DOKEZO: Hii pizza inatengenezwa kama ilivyoelezwa hapa. Mapishi haya ya pizza ni muendelezo wake kwa kuweka vionjo tofauti ili kuleta ladha. Muda uliokaridiwa hapa ni kuivisha pizza na sausage. Ukitaka kupika kuanzia mwanzo tafadhali angalia muda kwenye mapishi haya ambayo ni original recipe. 

 • Wakati umeshamaliza kuandaa pizza, kata sausage kwenye vipande vidogo.

pizza-2

 • Pasha moto oven kwenye nyuzi 250°C kwa muda wa dakika 5 hai 7.
 • Weka sausage juu ya pizza kwa kuzisambaza vizuri ili zisipandiane. Hii inarahisisha kuiva vizuri na kujishika kwenye pizza

pizza-4

 • Weka pizza yako kwenye oven, ukitega muda wa dakika 7 hadi 15. Angalia mara kwa mara ili isiungue

pizza-5

 • Pizza ikishaiva, toa, weka pembeni. Unaweza kuikata vipande na kusubiria ipoe kabla ya kuanza kula.

pizza-1

Jirambe na utamu wa pizza, usisahau kushare na wenzio ili wapate kujiramba pia.


MAPISHI YAPENDWAYO

Salad yenye sausage
dakika 5
Walaji: 1

Supu ya Kuku
dakika 30
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.