Pizza yenye topping ya kuku na cheese

Pizza, chakula rahisi kuandaa unachoweza kula wakati wowote - asubuhi, mchana au usiku. Ni vizuri kuandaa siku unayotaka kula chakula na kupumzika vizuri ukiwa unaongea na familia, marafiki au wengine Ni chakula chepesi, chenye virutubisho vingi na pia ni kitamu sana. Unaweza kuongeza vitu unavyopenda kuipendezesha pizza yako. Mapishi haya yameandaliwa na @nnjosie, asante kwa kutushirikisha kwenye kujiramba na utamu wa misosi.

Mahitaji

Kwa ajili ya unga:

 • Vijiko 2 vya chai vya hamira (yeast)
 • Vikombe 1 ¾ vya unga wa ngano. Tenganisha, weka kidogo pembeni
 • ¾ ya kikombe cha maji ya uvuguvugu
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • ½ kijiko cha mafuta ya Olive (Mafuta ya mizeituni)

Kwa ajili ya topping:

 • Minofu ya kuku
 • Mixed  herbs vijiko 2 vya chakula
 • Nyanya 2 kubwa
 • Pilipili hoho 1 na nusu
 • Mozzarella cheese
 • Kitunguu saumu vijiko 3 vya chakula vilivyosagwa
 • Butter vijiko 2 vya chakula
 • Pilipili manga kijiko 1 cha chai

 

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Mapishi haya ya pizza unayoweza kuandaa kirahisi nyumbani yameandaliwa na @nnjosie. Kwa ujumla pizza hii imeandaliwa kwa kufuata maelezo kama ilivyoandikwa hapa, lakini imetumia topping ya kuku, butter, mozarella na pilipili manga.

 • Pasha oven nyuzi joto 350°F (180°C). Bandika minofu ya kuku jikoni, acha ichemke kwa dakika 15. Weka pembeni ipoe.
 • Kwenye kikango, weka butter acha iyeyuke, kisha weka kitunguu saumu kijiko 1, mixed herbs na pilipili manga. Epua acha ipoe weka kwenye friji kwa muda.
 • Sambaza butter iliyotoka kwenye friji juu ya pizza kwa tumia kijiko. Weka kuku, nyanya, pilipili hoho kisha nyunyizia kitunguu saumu. Weka mozzarella cheese na nyunyizia mixed herbs. Oka Pizza kwa dakika 15 mpaka 20.
 • Epua. Jirambe.

misosi-pizza


Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.