Pizza yenye toppings za marguez na pilipili

Hii ni aina nyingine tofauti ya kuandaa Pizza yenye marguez, olive na pilipili. Marguez ni sausage za ng’ombe au kondoo zenye viungo mbalimbali. Ni tamu kutumia kuandaa pizza kama hii. Hii pizza ni tamu maana ina viungo mbalimbali, unapata ladha tamu na unashiba kwa muda mrefu. Hii pizza ina vitunguu, nyanya, zaituni, marguez, pilipili za kijani na mafuta ya zaituni.

Mahitaji

Kwa dida la pizza:

 • Unga wa ngano gramu 300
 • Hamira kijiko 1
 • Maji ya uvuguvugu
 • Chumvi
 • Zaituni 10
 • Mafuta ya zaituni (Olive oil)

Kwa topping:

 • Nyanya 5 zilizomenywa na kukatwa vipande
 • Vitunguu 3 vimenywe na kukatwa vipande
 • Pilipili 3 za kijani
 • Nyanya ya kopo (tomato paste) vijiko 2
 • Sukari vijiko 3
 • Mafuta ya kula
 • Merguez 2
 • Mozzarella cheese zilizokwanguliwa gramu 150g
 • Chumvi
 • Pilipili, si lazima ila ni vizuri kama utaongezea kuboresha ladha ya pizza

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Hii ni pizza unayotakiwa kuandaa na kuila mara baada ya kuiva, maana inakuwa tamu na bora kama ikiliwa bado ya moto.

 • Chekecha unga wa ngano kwenye chombo safi. Ongeza chumvi na hamira iliyochanganywa kwenye maji ya uvuguvugu. Ongeza maji taratibu kisha anza kukanda unga kwa mikono. Kanda kwa muda wa dakika 20 hadi dida (unga uliokandwa) liwe sawia na kulainika vizuri. Tengeneza kwenye umbo la mpira, funika na kitambaa na acha pembeni lipate kuumuka.
 • Andaa zaitiuni (Olives) kwa kuzikata  kwenye vipande vidogo. Weka vipande vya zaituni kwenye bakuli iliyo na mafuta ya zaituni (olive oil) kisha koroga mchanganyiko vizuri kisha weka vipande vya olive kwenye dida (unga uliokandwa), tandaza vizuri ili ziendee kwenye dida. Acha dida liendelee kuumuka kwa muda wa dakika 10 zaidi.
 • Bandika kikaango au sufuria jikoni, weka mafuta ya kula na acha yapate moto. Weka nyanya zilizokatwa vipande pamoja na nyanya ya kopo (tomato paste), koroga pamoja. Ongeza chumvi na pilipili, koroga pamoja. Punguza moto uwe wastani hadi maji yote yatoke kwenye sauce ya nyanya. Ongeza maji kiasi, kama vijiko 4 vikubwa na koroga vizuri pamoja.
 • Bandika chombo tofauti jikoni, weka mafuta na acha yapate moto vizuri. Weka kitunguu maji, koroga na acha kiive hadi kiwe na rangi ya kahawia. Ongeza chumvi na pilipili kisha koroga pamoja. Ongeza sukari kiasi, koroga.
 • Tandaza dida kwenye sehemu unayotumia kukandia iliyo na unga kiasi. Kata kwenye maumbo ya duara mfano wa pizza (kulingana na ukubwa wa oven unayotumia kupikia pizza).
 • Washa oven kwenye nyuzijoto 200°C (392°F), acha ipate moto vizuri.
 • Weka dida lililo tayari kwenye sehemu iliyopakwa mafuta, acha iumuke kwa dakika 10 zaidi. Muda ukitimia, toboa matundu madogo na uma kisha tandaza sauce ya nyanya juu yake. Tandaza pia vipande vya sausage, vitunguu na pilipili za kijani juu yake. Mwagia cheese ya mozzarella iliyokwanguliwa juu ya pizza.
 • Weka pizza kwenye oven, acha hadi iive – takribani dakika 35 hadi 45. Uwe unaangalia mara kwa mara ili isiungue.
 • Pizza ikishaiva toa na kula wakati bado ya moto.

pizza-misosi-3


MAPISHI YAPENDWAYO

Kuku wa limao
dakika 45
Walaji: 4

Mkate wa kuku na mayai yake
dakika 40
Walaji: 4

Viazi vya mboga mboga
dakika 18
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.