Polish dipped potatoes

Viazi vya kuchovya kwenye unga wa ngano na mayai ni chakuka rahisi kuandaa na kitamu. Unaweza kula viazi hivi kwa viambato tofauti – nyama, njegere, nyama choma, kuku, ng’ombe au vyakula vingine upendeleavyo. Ni chakula unachoweza kula wakati wowote, kwa kutofautisha kiwango kutokana na muda.

Mahitaji

 • Viazi mbatata kilo 1 (ulaya)
 • Mayai 3
 • Unga wa ngano ¼ kilo
 • Maziwa 200mls
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Mafuta ya kula ½ lita

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kwenye viazi hivi unaweza kuongeza pilipili manga, kitunguu saumu, tangawizi na viungo vingine unavyopendelea kwenye chakula.

misosi-polish-dipped-potato-00

 • 1 Andaa viazi – menya, kata katikati au mara mbili kama kiazi kikubwa. Osha kisha weka kwenye sufuria yenye maji na Chumvi kidogo sana (usiweke Chumvi nyingi, maana utaweka Chumvi kwenye mchanganyiko wa mayai). 
 • 2 Bandika jikoni, acha viazi vichemke hadi viive. Kuwa muangalifu visiive sana hadi kulainika na kuanza kuvunjika. Viazi vikishaiva, toa kwenye maji, acha pembeni ili vipoe na kukauka maji. Unaweza kutumia chujio kubwa la chakula kuchuja maji kirahisi.
 • 3 Kwenye bakuli kavu, weka unga wako wa ngano, maziwa (kama hakuna maziwa unaweza kutumia maji ya baridi) na chumvi kidogo. Koroga mchanganyiko vizuri na whisker ili kuondoa mabonge ya unga. Ongeza ute na kiini cha yai kwenye mchanganyiko huku ukiendelea kukoroga hadi upate uji mzito ulio laini. Hifadhi kando.
 • Injika sufuria ya mafuta yako utakayotumia kukaangia viazi. Acha yapate moto vizuri.
 • 4 Tenga viazi vichache, tumbukiza kwenye mchanganyiko wa mayai na unga wa ngano. Hakikisha vimefunikwa vizuri na Uji Uji. Kwa kutumia kijiko kikubwa, au upawa, chota kiazi kimoja kimoja na uweke kwenye sufuria ya mafuta yaliyopata moto. Rudia haua hii kwa viazi vilivyobakia kulingana na ukubwa wa sufuria. Acha viazi vikaangike taratibu, huku ukiwa unageuza kila upande hadi vipate rangi ya udhurungi (golden brown). Toa viazi kwenye mafuta na weka kwenye bakuli au chombo kikubwa kilichowekwa karatasi ya kunyonya mafuta (kitchen towels au paper towel) ili kukausha mafuta kwenye viazi.
 • 5 Rudia zoezi la kukaanga hadi umalize viazi vyote.
 • 6 Viazi vitakuwa tayari kuliwa. Unaweza kula viazi hivi na kuku,nyama ya kuchoma,mbogamboga au kachumbali.

misosi-polish-dipped-potato-steps


MAPISHI YAPENDWAYO

Kuku wa kuoka
saa 1
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.