Pound cake

Keki ni chakula chenye ladha tamu sana. Unaweza kunywa na chai au kinywaji chochote kama maji, juice na soda au ukala yenyewe na bado ukafurahi.

Mahitaji

 • Butter isiyokua na chumvi kikombe 1
 • Mayai 6
 • Sukari nyeupe vikombe 3
 • Unga vikombe 3
 • Vanila vijiko 2 vya chai
 • Chumvi nusu kijiko cha chai
 • Maziwa kijiko 3 vya chakula
 • Baking powder kijiko 1 cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Washa oven lipate joto kwa nyuzi 165C.
 • Chukua bakuli weka sukari na butter, koroga sukari na butter mpaka vilainike.
 • Weka mayai huku ukiendelea kuchanganya.
 • Weka unga, baking powder na chumvi changanya kwa nguvu ili vichanganyikane vizuri.
 • Weka vanila, changanya mpaka uone mchanganyiko huo si mwepesi sana wala mzito.
 • Ongeza maziwa,koroga ili mchanganyiko uchanganyike vizuri ila usikoroge sana mana keki inaweza kua ngumu.
 • Paka butter kwenye chombo cha kuokea. 
 • Kisha mimina mchanganyiko kwenye chombo ulichopaka butter.
 • Weka kwenye oven na uoke keki kwa lisaa 1, itakua ya kahawia chukua toothpick choma kuona kama imeiva, toothpick ikiwa kavu hapo imeiva.
 • Iache ipoe kwa dakika 15 anza kujiramba.

MAPISHI YAPENDWAYO

Kabeji yenye royco
dakika 10
Walaji: 4

Samaki wenye sauce ya pilipili
dakika 35
Walaji: 4

Maandazi ya apple
dakika 5
Walaji: 5

Tambi za maziwa na iliki
dakika 15
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.