Roast tamu ya ng'ombe na viazi

Roast ya nyama ya ng'ombe na viazi ni chakula chepesi na kizuri wakati wowote unaopenda kula chakula kizuri na kuridhika bila kuvimbiwa. Pata protini, madini ya chuma, vitamini na madini tofauti kwenye chakula hiki. Uwepo wa viungo unakupa ladha tamu, harufu nzuri na raha ya kila kijiko kinachoingia mdomoni kwako.

Mahitaji

 • Karoti 1 kubwa, kata vipande vikubwa
 • Giligilani kiasi
 • Vitunguu maji 3 vikubwa
 • Soy sauce kijiko 1 cha chai
 • Pilipili 1
 • Curry powder kijiko 1 cha chai
 • Nyama yenye mafuta kiasi kilo 1
 • Pilipili hoho 1, kata vipande vikubwa
 • Chumvi kiasi
 • Tangawizi kipande 1 wastani
 • Ndimu 1
 • Kitunguu saumu 1
 • Nyanya 2
 • Broccoli
 • Viazi mbatata 4

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuwa huru kuongeza au kupunguza mahitaji kulingana na unavyopenda

 • Kata nyama vipande vya wastani, osha alafu ibandike jikoni weka chumvi kiasi, ndimu na tangawizi. Pika kwa dakika 30 mpaka nyama iive lakini isilainike. Hakikisha maji yameisha yamebaki mafuta.
 • Katia kitunguu maji, pika ukigeuza mpaka kitunguu kiive. Weka pilipili hoho, karoti, broccoli. Pika kwa dakika 5 kisha weka soy sauce, curry powder, pilipili, nyanya na saumu. Hakikisha nyanya zimeiva vizuri.
 • Nyama ikiwa tayari epua, weka pembeni. Menya viazi, osha vizuri kata katikati, weka chumvi, kwagulia kitunguu maji juu ya viazi. Kisha vikaange.
 • Pakua nyama weka kwenye bakuli, weka giligilani juu kisha weka viazi kuzunguka sahani kama picha inavyoonyesha.
 • Pishi letu waweza kujiramba na chakula chochote. Changamsha mdomo.

misosi-nyama-viazi


MAPISHI YAPENDWAYO

Cookies za limao na mayai
dakika 15
Walaji: 5

Roast ya Samaki
dakika 30
Walaji: 3

Chips za kuoka zenye viungo
dakika 40
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.