Roast ya kuku, nazi na maziwa

Unaweza kula mboga hii pamoja na wali, ugali au kuchanganya na macaroni au tambi. Kizuri zaidi ni ladha ya kipekee unayoipata kutokana na mchanganyiko wa viungo

Mahitaji

 • Kuku-1/2
 • Nyanya 4
 • Sour cream (au Maziwa ¼ lita)
 • Nazi ½ kifuu
 • Kitunguu 1
 • Curry powder kijiko 1 cha mezani
 • Chumvi kijiko kidogo cha chai
 • Kitunguu swaumu 1
 • Tangawizi 1
 • Carrot 1
 • Viazi mviringo (Uiaya) 3
 • Pilipili hoho 1
 • Limao (au ndimu) 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 •  Tayarisha kuku kwa kukata vipande vinavyokutosha na kuosha nyama.
 • Tayarisha tangawizi kwa kuiponda hadi ilainike.
 • Weka chumvi, tangawizi kwenye kuku kisha nyunyuzia limao. Koroga mchanganyiko. Acha mchanganyiko ukae kwa takribani dakika 15 ili kuruhusu viungo kumlainisha kuku kabla ya kuanza mapishi.
 • Andaa pilipili hoho, kitunguu, viazi na nyanya. Menya viazi na kata vipande vidogo vidogo vitakavyoiva kirahisi. 
 • Bandika kuku jikoni. Usiongeze maji hata kidogo kwenye kuku. Acha achemke na maji ya kuoshea. Weka moto wa wastani. Acha ichemke hadi maji yakaukie ila angalia isiungue ( Itachukua takribani dakika 10-15).
 • Ongeza maji kama ½ lita ili nyama iive vizuri. Ongeza viazi kwenye mchanganyiko huu ili viive na nyama. Acha vichemke kwa dakika 10 - 15.
 • Anza kutengeneza sauce yako kwa kuweka mafuta kwenye sufuria, yakishapata moto weka kitunguu. Subiria hadi kiwe cha brown halafu weka kitunguu saumu. Baada ya kuiva kiasi weka nyanya. Funika kwa muda hadi nyanya zichemke kiasi (dakika 7 hadi 10).
 • Ongeza pilipili hoho na carrot.
 • Ongeza curry powder kipimo cha kijiko kikubwa cha mezani. Kisha koroga mchanganyiko.
 • Ongeza tui la nazi, kisha koroga taratibu hadi ianze kuchemka ili kuzuia tui lisikatike.
 • Ongeza sour cream (au maziwa) kwenye mchanganyiko wako. Kisha koroga.
 • Acha mchanganyiko uchemke kwa muda wa dakika 5 hadi 7.
 • Changanya nyama na viazi pamoja na mchanganyiko wa sauce yako. Koroga kidogo kisha acha mchanganyiko wako uchemke kwa muda wa dakika 5 hadi 7 ili kuiva.

 

Jirambe  . Ukimaliza kujiramba, tutumie maoni yako hapa. Kuwa na upendo, bofya kushare na wenzio ladha ya maisha.

 

 


Toa maoni yakoMisosi Team
10:59, Mon 17 Mar 2014
Unaweza pia kuongeza vikorombwezo unavyopenda kwenye haya mapishi. Ni vizuri kama utakuwa na kachumbari ambayo italeta rangi na hamu ya kula. Mie hupendelea kula na tango, nyanya, pilipili hoho na karoti. Rangi ya nyanya huwa inanipa hamu ya chakula sana.
JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.