Roast ya maini

Maini ni chanzo kikubwa cha virutubisho muhimu mwilini. Roast hii hii ya maini inaweza kuliwa na wali, ugali, au pamoja na chapati. Kuna kila aina ya sababu za kula mboga hii bora na familia yako.

Mahitaji

 • Maini ½ kilo
 • Nyanya 4
 • Kitunguu 1
 • Karoti 1
 • Pilipili hoho 1
 • Ndimu 1
 • Chumvi
 • Mafuta ya kula

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Anza kutayarisha ini kwa ufasaha. Ondoa tabaka (ngozi ya juu) ya ini ambayo huwa hailiwi. Osha na kata vipande kwenye ukubwa unaopenda.
 • Nyunyuzia ndimu kwenye vipande vya ini na kisha weka chumvi. Changanya vizuri ili vipande kuchanganyika sawia.
 • Andaa viungo kwa kuosha na kuvikata vipande vidogo – nyanya, pilipili hoho, karoti na vitunguu.
 • Weka mafuta kwenye sufuria, chungu au kikaangio unachotumia kupikia maini.
 • Weka maini. Yakaange hadi yaive.
 • Weka kitunguu, koroga ili viive vizuri.
 • Weka pilipili hoho n a karoti. Koroga kwa dakika 1 hadi 2.
 • Weka nyanya. Koroga kiasi.
 • Kama chumvi haitoshi, ongeza chumvi. Koroga na kisha funika na mfuniko ili nyanya ziiive.
 • Baada ya dakika 5 – 8 unaweza kutoa mboga kwa kuwa imeiva.
 • Jirambe

MAPISHI YAPENDWAYO

Mchuzi wa biryani
dakika 35
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.