Roast ya nyama yenye nazi na maziwa

Nyama hii ina kila aina ya kionjo unachotaka kukipata kwenye chakula – nazi, viungo na maziwa (maziwa mgando au sour cream). Uwepo wa mboga za majani hukifanya hii mboga kuwa tamu zaidi. Nilifurahi wakati wa kula, maana ni chakula kitamu na chenye afya.

Mahitaji

 • Vitunguu maji 2, menya na kata vipande vidogo
 • Pilipili hoho (Nimetumia 2 za rangi tofauti), menya kata vipande
 • Tui la nazi kikombe 1 (Kama hutumii nazi unaweza kutumia karanga)
 • Maziwa ya mgando (sour cream) ½ kikombe
 • Nyama ½ kilo (Nyama mchanganyiko itakuwa vizuri kuleta supu)
 • Karoti 2, zimenywe na kukatwa vipande vidogo
 • Chumvi
 • Viazi mbatata 4, menya kata katikati, hifadhi kwenye maji
 • Bamia 6, kata ncha, pasua katikati
 • Nyanya chungu 3 – chemsha kwa dakika 5, toa Maganda na hifadhi pembeni.
 • Nyanya 4 (Au tomato paste), menya, kata vipande vidogo au saga ikiwezekana
 • Kitunguu saumu 1, menya, ponda vizuri.
 • Tangawizi 1, imenywe, isagwe vizuri
 • Mafuta ya kula (nimetumia mafuta ya zaituni – olive oil)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Ukimaliza kuandaa, mboga itakuwa inaonekana hivi:

misosi-nyama-maziwa-main2

 • Kata nyama kwenye vipande vya wastani. Osha kisha weka chumvi, tangawizi na kitunguu saumu kidogo sana ili kuweka ladha. Usitumie kitunguu saumu chote, kitatumika kwenye kupikia. Bandika nyama jikoni, usiongeze maji. Acha ichemke hadi maji yake yakauke. Maji yakikauka, ongeza maji mengine, weka viazi mviringo kwenye nyama ili viive pamoja. Acha nyama iive vizuri.
 • Chemsha nyanya chungu kwenye sufuria yenye maji kiasi. Zikiva, menya ngozi ya juu na hifadhi pembeni.
 •  Bandika sufuria au kikaango jikoni, weka mafuta ya kula kiasi. Yakichemka weka kitunguu saumu, koroga. Weka kitunguu maji. Koroga, acha viive na kulainikia kiasi – takribani dakika 3. Ongeza chumvi kiasi. Ongeza nyanya, koroga kiasi kisha funika acha ziive vizuri.

Kama unatumia nyanya fresh unaweza kuziponda baada ya kuiva kiasi ili zilainike na kuwa uji baada ya muda, kama ni tomato paste acha ziive tu. Hakikisha hazikauki na kuungua tu, unaweza kuongeza maji kiasi au supu ya nyama ili ziendelee kuiva vizuri.

 • Baada ya dakika kama 8 hadi 10 baada ya nyanya kuchemka, ongeza pilipili hoho na karoti. Koroga vizuri kisha funika.

Mie huwa napenda pilipili hoho na karoti zisiive sana ili nipate virutubisho zaidi na pia harufu nzuri ya pilipili hoho. Kama unapendelea ziive vizuri unaweza kuweka mapema ili zikae jikoni muda mrefu, lakini unapunguza virutubisho kwa kuziweka muda mrefu kwenye moto.

 • Sauce ya nyanya ikishaiva changanya nyama iliyoiva na supu yake. Weka nyanya chungu. Koroga pamoja vizuri. Weka tui la nazi. Koroga hadi tui lianze kuchemka, kisha funika kwa dakika 5 ili tui lichanganyike na chakula.
 • Weka maziwa ya mgando (sour cream) kisha koroga vizuri ili lipate kuchanganyika. Acha ichemke kwa dakika 3 hadi 5. Epua chakula kitakuwa tayari kuliwa.
 • Hii mboga inaweza kuliwa pamoja na vitu vingine mfano mkate, chapati, maandazi, au hata wali na ugali. Ni chaguo lako.
 • Jirambe na roast ya nyama

misosi-nyama-maziwa-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Viazi na nyama ya kusaga
dakika 20
Walaji: 2

Nyama yenye curry sauce
dakika 25
Walaji: 6

Visheti vya vanilla na mdalasini
dakika 15
Walaji: 10

Chicken Tandoori
dakika 60
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.