Roast ya Samaki

Huyu ni samaki anayepikwa kama supu, maana hakaangwi kabla ya kuwekwa kwenye mchuzi. Ni samaki anayebaki na virutubisho muhimu vyote, akiwa analeta afya tele. Mboga hii haina mafuta mengi, na inaweza kuliwa na vyakula tofauti.

Mahitaji

 • Samaki mbichi 1
 • Binzari nyembamba ½  kijiko kidogo
 • Mdalasini kijiko 1 kidogo (au vipande 2 vya miti)
 • Tangawizi ya unga ½ kijiko kidogo
 • Samaki masala kijiko 1 kidogo
 • Pilipili manga ½ kijiko kidogo
 • Curry powder kiasi
 • Mbegu za korianda kijiko 1 kidogo
 • Nyanya 4
 • Nyanya paste kijiko 1 kikubwa
 • Hing ½ kijiko
 • Karoti 1, menya kisha kata vipande vidogo
 • Kitunguu maji 1
 • Kitunguu saumu 1
 • Ndimu 1
 • Mafuta vijiko 2 vya chakula
 • Chumvi

 

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Safisha samaki – toa magamba, toa utumbo kisha osha vizuri. Kama samaki mkubwa sana kata vipande vya wastani. Hifadhi vizuri.
 • Menya kisha kata kwenye vipande vidogo – nyanya, kitunguu saumu, kitunguu maji. Hifadhi pembeni.
 • Bandika sufuria jikoni. Weka mafuta, yakipata moto weka kitunguu saumu na kitunguu maji. Pika kwa dakika 3 huku ukikoroga mara kwa mara. Moto uwe wa wastani.
 • Weka karoti na viungo vingine vyote kasoro nyanya. Koroga pamoja vizuri kisha weka nyanya. Funika ili nyanya ziiive.
 • Weka za kopo, koroga kisha weka chumvi. Acha zichemke kwa dakika 3 hadi 5.
 • Weka samaki, kamulia ndimu juu yake. Ongeza maji funika ili samaki apate kuiva. Takribani dakika 15 hadi 20.
 • Samaki akishaiva, epua mboga ujirambe.

misosi-fish-roast-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Supu ya ulimi wa ng'ombe
dakika 40
Walaji: 1

Kuku wa kukaanga wa ndimu
dakika 10
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.