Salad ya kabichi

Mahitaji

 • Kabichi 1
 • Pilipili hoho 1
 • Karoti 2
 • Vitunguu maji 2
 • Kitunguu saumu 1
 • Limao au ndimu
 • Tangawizi 1
 • Mafuta vijiko 3 (olive oil)
 • Chumvi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Katakata kabichi, pilipili hoho, karoti, kitunguu maji. Twanga kitunguu saumu na tangawizi.
 • Osha kabichi, iweke ichuje maji alafu inyunyizie chumvi.
 • Changanya pilipili hoho, karoti na kitunguu maji kwenye kabichi.
 • Kamulia limao au ndimu.
 • Bandika sufuria, weka mafuta yakipata moto weka kitunguu saumu na tangawizi.
 • Koroga mpaka viive, weka kabichi koroga kwa muda wa dakika 5. Epua halipendezi likiiva sana, hapo ni muda wa kujiramba.

MAPISHI YAPENDWAYO

Supu ya ulimi wa ng'ombe
dakika 40
Walaji: 1

Kuku wa kukaanga wa ndimu
dakika 10
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.