Salad ya macaroni na maziwa ya mgando

Nilikuwa na hamu ya kula chakula laini, chenye afya. Kutokana na kuwa peke yangu, hiki kilikuwa chakula mahsusi na kitamu cha kufanya usiku wangu uwe murua sana. Kizuri zaidi, sikuwa na haja ya kutumia kitu chochote cha moto, nimekula chakula hiki kwa macaroni ya baridi na maziwa ya mgando (yoghurt) baridi. Unaweza kushangaa, lakini ni afya kula chakula cha wanga cha baridi.

Mahitaji

  • Nyanya 1
  • Nyama stake ¼ kilo (nyama si lazima, ila ni vizuri kama ukiwa nayo kama kiambato cha chakula)
  • Tango ½
  • Macaroni yaliyopikwa na kuwekwa kwenye jokofu (nusu paketi yanatosha). Unaweza pia kuwa na macaroni ya moto, siyo mbaya, ili mradi upate kula na ladha tamu.
  • Mtindi au maziwa ya mgando (Yoghurt) – (¼) robo lita.

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

  • Tengeneza nyama – kata vipande vidogo sana, kisha osha vizuri. Weka chumvi. Bandika chungu jikoni, weka mafuta ya kula. Subiria yapate moto, weka nyama kwa muda wa dakika 5 hadi 10. Ikaange kwa kuigeuza na kisha itoe.
  • Changanya nyama na mtindi. Koroga vizuri ili vipate kuchanganyika. 

Unaweza pia kuwa na mtindi wa kawaida wenye sukari, huleta ladha nzuri ya mchanganyiko wa sukari na chumvi kwenye chakula.

  • Andaa macaroni kwenye sahani. Mwagia maziwa ya mgando.
  •  Kata kachumbari yako ya nyanya na tango. Unaweza kuongeza vingine unavyotaka, mfano karoti na pilipili hoho.
  • Unaweza kujiramba.

Nimekula chakula hiki kwa macaroni ya baridi kutokana na ushauri wa kiafya uliotolewa kwenye makala hii hapa.


MAPISHI YAPENDWAYO

Kuku wa kuoka
saa 1
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.