Salad ya mahindi na samaki

Hiki chakula ni kitamu lakini pia ni chakula bora. Unapata virutubishi vya omega 3 toka kwenye samaki. Unapata wanga toka kwenye mahindi (Siyo nyingi kama ukila ugali). Unapata pia virutubisho toka kwenye nyanya, tango na mboga za majani. Utapitisha mchana wako vizuri ukiwa umekula chakula bora sana.

Mahitaji

 • Punje za mahindi yaliyochemshwa 200g
 • Tango 1
 • Kitunguu 1
 • Salad (chaguo lako)
 • Samaki (hapa tumetumia tuna wa kopo)
 • Vinegar (Inatumika mbadala kwa chumvi)
 • Nyanya 2

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 

Tuna andaa salad yetu ya mahindi na samaki itakayokuwa kama hivi. 

salad-

 • Changanya majani ya salad unayopendelea. (Osha kwanza kama bado hayajaoshwa. Ila angalia usiyaminye)
 • Kata kitunguu kwenye bakuli tofauti, kisha osha na maji. Ukimaliza nyunyizia vinegar kwenye kitunguu, koroga vizuri ili ichanganyike. Ukimaliza changanya kwenye salad.

Mie huwa naosha kitunguu ili kupunguza makali. Maana kitunguu kina asidi ya kiwango kikubwa sana. Usipoangalia unaweza kuwa unalia wakati unakula chakula.

 • Kata  nyanya, changanya kwenye salad pamoja.
 • Kata tango, changanya kwenye salad. Mie huwa simenyi maganda, napenda nile na maganda yake, naona inapendeza zaidi.
 • Weka samaki kwenye salad. Hapa nimetumia samaki aina ya tuna wa kutoka kwenye kopo. Unaweza kutumia samaki unayependelea.
 • Tandaza vizuri punje za mahindi kwenye salad yako
 • Mwagia vinegar kama unavyopendelea na ujiandae kujiramba.

salad-2

 


MAPISHI YAPENDWAYO

Couscous
dakika 100
Walaji: 4

Chips na kuku
dakika 45
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.