Salad ya samaki

Je uko kwenye kipindi cha kupunguza mwili? Basi hapa ndio mahali pako. Salad ni chakula bora, sababu unakula zaidi mboga majani na vitu asilia. Unaweza kuandaa salad hii ikiwa kavu na pia unaweza kuongeza nyama, samaki, mayai, sausage au vinginevyo. Kwa matokeo mazuri zaidi, kula ikiwa yenyewe tu ili upate kula vyakula asilia zaidi.

Mahitaji

Mahitaji ya Samaki

 • Samaki 1
 • Kitunguu saumu
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • Limao au ndimu 1
 • Pilipili manga
 • Tangawizi 1

Mahitaji ya salad

 • Vitunguu maji 2
 • Tango 1/2
 • Nyanya 2
 • Pilipili hoho
 • Vinegar
 • Karoti
 • Salad (Aina yeyote utakayochagua)

20150110_194431

 

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Leo tuna andaa salad ambayo itakuwa kama hivi ikishakamilika:

20150110_200353

 • Andaa samaki kama ilivyoelekezwa kwenye mapishi hapa.
 • Anza maandalizi ya salad kwa kuosha pilipili hoho, karoti. Menya kitunguu na kisha osha vizuri. Osha salad vizuri kwa kuweka kweye chombo kinachopitisha maji. Usibinye wala kuikata, maana majani yatasinyaa. Osha taratibu bila kuharibu.
 • Kata kitunguu kwenye chombo pembeni. Osha kitunguu chako ili kupunguza ukali wake, maana hapa kinaliwa kibichi.
 • Weka vinegar na chumvi kwenye kitunguu. Koroga vizuri.
 • Andaa salad kwenye sahani. Tandaza vizuri.
 • Weka mchanganyiko wa kitunguu na vinegar.
 • Kata tango juu ya salad. Kata karoti juu ya salad. Changanya taratibu ili vipate kuwa mchanganyiko mzuri.
 • Kata nyanya kisha weka kwenye salad.

20150110_200217

 • Weka kipande cha samaki, au samaki mzima juu ya salad na kisha nyunyizia vinegar.

20150110_200238

20150110_200353

 • Jirambe

MAPISHI YAPENDWAYO

Samaki wa kupaka
dakika 60
Walaji: 2

Cheese Burger
dakika 15
Walaji: 4

Polish dipped potatoes
dakika 15
Walaji: 6

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.