Salad ya tango, nyanya na chungwa

Je ulishawahi kupenda kula vitu vichache ambavyo hukufanya ushibe bila kula vyakula vyenye karoli (Calories) nyingi? Basi hili ni chaguo tosha kwako. Mie nimeamua kupunguza kidogo mwili, hivyo nakula vyakula vyepesi kwa muda ili nipate uzito ninaoupenda. Si vibaya kama utajaribu, maana nakula vyakula vinavyonifanya nishibe, ila kwa kula virutubisho visivyohifadhiwa kwa wingi mwilini. Hiki ni chakula kimojawapo kwenye orodha yangu. Karibu kama utapenda .

Mahitaji

 • Tango ½
 • Chungwa 1
 • Karoti (siyo muhimu sana kwa haya mapishi)
 • Chachandu
 • Chumvi
 • Vinegar

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuandaa salad hii ni rahisi sana maana huna haja ya kupika. Hapa ni muda wako tu wa kuandaa na kisha kuanza kula. Faida za hiki chakula ni kuwa, unapata Vitamin C na fiber (Chungwa), unapata vitamins A and C and folic acid (Nyanya), na vitamin K, B vitamins, copper, potassium, vitamin C, na manganese (Tango). Hivi vyote hukusaidia kuepukana na magonjwa mengi sugu ikiwemo saratani (cancer) na mengine mengi. Pia husaidia kuboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula mwilini mwako.

20150109_233113

Bado hujashawishika kula hivi?

Hivi ndivyo jinsi ya kuandaa:

 • Osha nyanya, na tango.
 • Kata nyanya, kwenye vipande vidogo.
 • Usimenye tango, kata vipande vidogo na majani yake. Majani ya tango ni mazuri kuyala, hivyo usiyatoe.
 • Menya chungwa. Hakikisha unaacha lile gamba jeupe baada ya kutoa ngozi ya nje. Linasaidia kuboresha mmeng’enyo wa chakula mwilini mwako.
 • Changanya vitu kwa pamoja. Kisha unaweza kuongeza chumvi.
 • Kama unapenda pilipili ongeza kiasi.
 • Unaweza pia kuweka vinegar badala ya chumvi ili kuipa salad yako ladha nzuri zaidi.
 • Unaweza kula hii salad na maji. Kama umeamua kula vyakula bora, punguza vinywaji vyenye kemikali kama soda na pombe. Maana utakuwa unafanya kazi bure kula vizuri wakati bado unakula sukari na kemikali nyingine.

20150109_233826

20150109_233059

 

Oops!! Kabla sijahau, chakula hiki ni kizuri zaidi kula usiku. Maana usiku ni wakati wa kula vyakula vyepesi ili usishibe sana.


MAPISHI YAPENDWAYO

Roast tamu ya ng'ombe na viazi
dakika 35
Walaji: 2

Lasagna
dakika 150
Walaji: 6

Samaki wa mchuzi wa nazi
dakika 15
Walaji: 4

Nyama tamu ya kukaanga
dakika 60
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.