Salad yenye nyama ya kuoka

Salad ni chakula bora. Wengi wetu tunapenda kula salad kama chakula ili kuzuia kuongeza uzito. Haya mapishi yanaonyesha jinsi ya kuongeza vionjo kwenye salad kwa kula na nyama ya kuoka. Nyama ya iliyookwa ni afya na nzuri zaidi kula kwa kiasi na kwa hamu.

Mahitaji

 • Nyama ya ng'ombe ½ kilo (Unaweza pia kutumia mbuzi au aina tofauti)
 • Karoti 2 kata vipande vidogo
 • Tangawizi 1 imenywe na kusagwa
 • Vitunguu saumu 2 vimenywe na kusagwa
 • Pilipili hoho 2 - kijani na nyekundu - zikatwe vipande
 • Kitunguu maji kikubwa 1 kikatwe vipande vidogo
 • Salad (Chaguo lako la salad unayopendelea)
 • Nyanya 2
 • Pilipili manga
 • Olive Oil
 • Limao 1 lililokamuliwa
 • Tango 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Mapishi haya yanaandalikwa kwa hatua 2 muhimu - tunaandaa nyama halafu tunatengeneza salad wakati wa kula.

Tunataka kuandaa chakula kinachofanana na hiki hapa:

salad-nyama-2

1. Pika nyama

 • Pasha moto oven kwenye nyuzi 250°C na acha iwe ya moto kwa muda wa dakika 5 hadi 10.
 • Andaa nyama – kata vipande wastani, osha kisha weka kwenye bakuli ya kioo au chombo unachotumia kupikia kwenye oven.
 • Ongeza viungo – kitunguu saumu, tangawizi, pilipili manga. Changanya vizuri.
 • Weka chumvi, changanya vizuri. Kamulia limao, kisha changanya vizuri mchanganyiko.
 • Menya viazi, kata vipande. Changanya kwenye nyama.
 • Weka karoti, pilipili hoho, kitunguu maji na changanya vizuri.
 • Weka olive oil, changanya vizuri.

salad-nyama-3

Olive Oil inasaidia kuifanya nyama kuiva bila kuungua. Mafuta haya ni afya, na hayana madhara kama utaweka kwenye kiwango kidogo. Ila si lazima, unaweza kuacha kuweka na nyama ikatoka vizuri.

 • Weka mchanganyiko wa nyama na viungo kwenye oven.
 • Weka muda dakika 40. Angalia mara kwa mara kama nyama inaiva vizuri au inaungua, na geuza ili kuifanya iive kwa uwiano mzuri.

salad-nyama-5

2. Andaa Salad

 • Osha salad yako vizuri
 • Weka kwenye chombo kikubwa, kata kwenye vipande vidogo kwa kutumia mikono
 • Kata nyanya, tango kwenye vipande vidogo
 • Changanya salad, nyanya na tango

salad-nyama-4

 • Baada ya nyama kuiva, changanya kwenye sahani yenye salad

salad-nyama-2

Jirambe na ladha ya maisha.


MAPISHI YAPENDWAYO

Tambi na nyama ya kusaga
dakika 25
Walaji: 2

Chachandu ya embe
dakika 15
Walaji: 4

Bagia za kunde
dakika 7
Walaji: 4

Maandazi ya Vanila na Nazi
saa 1
Walaji: 15

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.