Salad yenye prawns (Kamba)

Salad yenye mchanganyiko wa prawns inafaa kuliwa wakati wowote,hasa usiku ili kuweza kula chakula chepesi na kuweza kulala vizuri. Ni vizuri kwa wale wanaopenda afya zao kwa kula chakula chenye ladha, wanashiba na kutopata madhara hapo baadae. Jirambe na utamu wa maisha kwa kuandaa hii salad rahisi.

Mahitaji

 • Kabichi
 • Nyanya
 • Vitunguu
 • Karoti
 • Spinach
 • Pilipilihoho
 • Olive oil
 • Limao au vinegar au ndimu
 • Chumvi kiasi
 • Apple
 • Prawns
 • Samaki aina ya salmon (wa kopo, maana ni rahisi kuweka kwenye salad)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Anza kutengeneza prawns. Toa maganda, waoshe, kisha nyunyuzia limao au ndimu. Wawekee viungo unavyopenda (mfano kitunguu saumu, pilipili manga, cube Maggie, mustard etc) kisha weka frying pan jikoni, mafuta na kaanga hadi waive.
 • Kata mboga za majani kwenye vipande vidogo. Weka kwenye sahani.
 • Kata nyanya, pilipili hoho, karoti kwenye vipande vidoho, kisha changanya na salad yako.
 • Changanya vinegar, limao au ndimu na olive oil pembeni kwenye bakuli. Unakoroga vizuri hadi ziwe sawia.
 • Nyunyuzia mchanganyiko wa limao au ndimu au vinegar na oil juu ya salad. Nyunyuzia kuzunguka salad, usirundike sehemu moja.
 • Weka prawns kwenye salad, koroga ili wachanganyike vizuri.
 • Weka salmon fish kwenye salad. Changanya zaidi ili upate uwiano bora.
 • Weka chumvi kiasi kisha anza kuchanganya changanya
 • Kumbuka, salad inaliwa ikiwa ya baridi, so huna haja ya kupasha moto.

Bon appetit ;)


MAPISHI YAPENDWAYO

Maandazi ya Mayai na Maziwa
dakika 20
Walaji: 4

Samaki wa kupaka
dakika 25
Walaji: 2

Tambi za hiliki na sukari
dakika 8
Walaji: 2

Ndizi za kuunga na nazi
dakika 20
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.