Salad yenye sausage

Je unapenda kula salad? Hii ni salad nzuri kwa wale wasiopenda kula tu majani bila nyama kidogo. Uwepo wa pilipili manga unakupa ladha tamu lakini vilevile unapunguza kasi ya kula na kukufanya ushibe haraka. Hivyo, hata kama chakula ni kidogo, utashiba vizuri.

Mahitaji

 • Salad (chaguo lako)
 • Kitunguu 1
 • Sausage (Hapa nimetumia sausage nene za ng’ombe, unaweza kutumia unazopendelea)
 • Vinegar (Nimetumia vinegar iliyochanganywa na mayonnaise kiasi)
 • Nyanya
 • Chumvi
 • Pilipili manga ya unga
 • Mafuta ya kula –  nashauri utumie olive oil (Mafuta ya zaituni).

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Menya kisha kata kitunguu kwenye vipande vidogo. Weka kwenye bakuli.
 • Bandika kikaango jikoni. Weka mafuta kiasi, acha yapate moto. Kata sausage kwenye vipande vyembamba. Weka kwenye mafuta, kaanga kwa dakika 3 hadi 5. Angalia zisiungue. Zikiiva zote hifadhi pembeni.
 • Bandika kikaango jikoni, weka mafuta ya kula. Acha yapate moto. Weka vitunguu. Ongeza pilipili manga. Kaanga kwa dakika 3 hadi 5, usiache kukoroga.  Vikilainika kiasi toa na weka kwenye bakuli. Mwagia vinegar. Koroga vizuri kwa pamoja.
 • Osha salad vizuri. Weka kwenye sahani. Weka saugage. Weka vitunguu vilivyo na vinegar. Kata nyanya kwa juu. Mwagia pilipili manga na kisha mwagia olive oil juu ya salad, hii itaipa ladha nzuri na tamu.
 • Unaweza pia kuongeza vitu unavyopenda – tango, karoti, pilipili na vingine.
 • Jirambe na ladha salad ya sausage.

Faida za hii salad:

Viungo kwenye chakula hukusaidia kupunguza kasi ya kula na kukufanya ushibe haraka. Ni chakula kizuri kwa kupunguza uzito. Chakula kama hiki kina kalori chache kutokana na kula majani. Pia mmeng’enyo wa majani mabichi tumboni hutumia kalori nyingi tofauti na vyakula vingine, hivyo husaidia mwili kupunguza uzito kwa kutumia mafuta yaliyohifadhiwa.


MAPISHI YAPENDWAYO

Chicken with mashed potato
dakika 30
Walaji: 1

Chicken tandoori
dakika 40
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.