Salad yenye yai na samaki

Leo tunaandaa salad, chakula chenye afya na unachoweza kula wakati wowote bila matatizo. Kama wewe si mpenzi wa nyama, unaweza kuacha kuandaa samaki na mayai na ukala chakula hiki vizuri bila matatizo.

Mahitaji

 • Samaki (nimetumia salmon)
 • Salad (chaguo lako, mie nimetumia majani  ya salad yaliyochanganywa)
 • Ndizi 2
 • Parachichi 1
 • Nyanya 2
 • Mayai 2
 • Chumvi
 • Pilipili manga
 • Kitunguu saumu
 • Mafuta ya kula (nimetumia olive oil)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Salad hii ni tamu, na vilevile ni bora. Mie nimeifurahia sababu napenda kula vitu vyepesi, hasa wakati wa usiku. Hivyo basi, ukimaliza salad yako itakuwa ina muonekano huu.

salad-samaki2

 • Pika samaki kama ilivyoelezwa hapa. Ndio nilivyomuandaa mimi kwenye hii salad.
 • Andaa mayai – pasua mayai kwenye bakuli, koroga. Weka chumvi, pilipili manga, kitunguu saumu. Koroga vizuri. Bandika kikaangio jikoni, weka mafuta. Yakipata moto, weka mayai. Acha yaive, geuza upande wa pili, yakishaiva ipua weka pembeni.
 • Andaa salad, weka kwenye chombo kinachoweza kupitisha maji, osha vizuri na kisha weka kwenye sahani.
 • Kata ndizi, weka kwenye sahani yenye salad. Menya parachichi, kata vipande vidogo, weka kwenye salad. Osha nyanya, kata vipande, weka kwenye salad.
 • Weka yai kwenye salad. Weka samaki.
 • Nyunyizia sauce unayoipenda, mie nimeweka pilipili na vinegar, maana napenda uchachu wake.
 • Jirambe.

saladndizi_main


MAPISHI YAPENDWAYO

Salad ya samaki
dakika 15
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.