Samaki, bamia, pilipili hoho na ugali

Chakula kitamu kinategemea sana upishi wako. Mfano, mie napenda sana samaki. Ni mboga niipendayo sana, hasa akiwa amekaangwa pamoja na viungo tofauti. Uwepo wa samaki na mboga za majani umefanya huu ugali uwe mtamu na ladha nzuri zaidi. Hiki ni chakula kizuri kwa wale wanaofanya kazi nzito wakati wa mchana. Uwepo wa viungo kama pilipili manga na kitunguu saumu hukifanya chakula kukushibisha mapema.

Mahitaji

Kwa samaki

 • Samaki vipande 4, andaa kwa mahitaji yako
 • Kitunguu saumu kijiko 1
 • Limao 1
 • Mafuta ya kula
 • Pilipili manga ½ kijiko
 • Chumvi
 • Tangawizi ya unga kijiko 1

Mboga za majani

 • Pilipili hoho 3 – rangi tofauti unazoweza kupata
 • Bamia 6
 • Kitunguu saumu cha unga ½ kijiko
 • Vitunguu 2
 • Mafuta ya kula (Olive oil ni chaguo zuri)
 • Chumvi
 • Pilipili za manga ya unga ½ kijiko
 • Kionjo cha mboga za majani (mfano royco, mchuzi mix, n.k)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Mboga yetu itaonekana kama hivi ikikamilika.

ugali-bamia-samaki-main

Maandalizi ya samaki

 • Andaa samaki – toa magamba, safisha vizuri kisha weka pembeni. Paka chumvi vizuri kwenye samaki.
 • Tengeneza marinade - changanya viungo vyote pamoja kasoro limao. Kisha changanya limao na koroga vizuri.
 • Paka marinade kwenye samaki, hakikisha imeenea vizuri. Acha samaki akae kwa muda wa dakika 10 hadi 15 ili iingie vizuri.
 • Weka kikaango jikoni, acha kipate moto vizuri. Weka mafuta ya kula. Acha yapate moto vizuri sana. Weka samaki, acha aive upande mmoja kisha geuza upande mwingine.
 • Samaki akishaiva, epua na weka pembeni

Maandalizi ya mboga ya majani

 • Kata kitunguu. Weka kwenye chombo pembeni. Kata karoti, tenga pembeni kwenye chombo. Osha bamia, kata na kisha weka kwenye chombo pembeni.
 • Weka sufuria au kikaangio jikoni. Ongeza mafuta na acha yapate moto vizuri. Weka kitunguu, koroga kiasi. Weka kitunguu saumu cha unga, koroga. Ongeza bamia na pilipili manga, koroga na funika kwa muda ili vipate kuiva kwa muda wa dakika 3 hadi 4. Weka pilipili hoho, kionjo cha mboga (royco, mchuzi mix, etc) na chumvi kisha koroga vizuri. Funika mchanganyiko kwa muda kiasi na mfuniko na acha ichemke vizuri kwa muda wa dakika 7 hadi 10. Geuza kidogo na kisha funika tena kwa dakika 3 hadi 5.

Unaweza kuongeza curry au tandoori ili kuipa mboga harufu nzuri na ladha bora zaidi.

 • Toa mboga na unaweza kula cha chakula unachopendelea.

ugali-bamia-samaki-other-poooor


Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.