Samaki na sauce ya bilinganya la kuoka

Bilinganya ni mboga inayoweza kupikwa kwa mapishi tofauti, haya ni aina mojawapo ya mapishi ya bilinganya ya kuoka kwenye oven. Uivaji wa bilinganya kwa mapishi haya ni mzuri sababu linaiva na kuwa laini na kuliwa kama sauce.

Mahitaji

 • Spinach
 • Pilipili manga
 • Bilinganya 1
 • Kitunguu saumu 1
 • Limao
 • Mafuta ya kula
 • Pilipili hoho 1
 • Chumvi
 • Tangawizi ya unga kijiko 1 kidogo
 • Karoti 1
 • Kitunguu maji kikubwa 1
 • Cayenne pepper 2
 • Samaki vipande 2 vilivyokaangwa

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kuongeza viambato unavyopenda kwenye mapishi haya ili kuongeza ladha. Kuwa huru na ongeza ubunifu wako.

misosi-samaki-bilinganya

 • Washa oven kwenye nyuzijoto 180°C, acha ipate moto wakati unaendelea kuandaa bilinganya.
 • Osha bilinganya vizuri, kisha toboa vitobo vidogo juu ya ngozi ya bilinganya kwa kutumia uma au kitu chenye ncha kali. Yawe matobo takribani kama 10 juu ya bilinganya. Paka mafuta ya kula juu yake kisha weka kwenye bakuli la kuokea.
 • Weka bilinganya kwenye oven, tega muda wa dakika 25 hadi 30 acha liive vizuri. Toa pale tu litakapokuwa limenywea na ngozi kusinyaa.

Wakati bilinganya linaiva, andaa sauce ya mboga za majani ili kuchanganyia na bilinganya likishaiva.

 • Andaa kitunguu maji na kitunguu saumu – menya kisha kata vipande vidogo. Osha kisha kata pilipili hoho na cayenne pepper vipande vidogo. Hifadhi pembeni.
 • Bandika kikaango jikoni. Acha kipate moto, kisha weka mafuta ya kula. Yakipata moto, weka kitunguu saumu, kitunguu maji na chumvi. Koroga vizuri hadi viive. Weka pilipili hoho na cayenne pepper kisha koroga vizuri. Acha viive. Kama kukiwa hakuna mchuzi, weka supu ya kuku kiasi kwenye mboga za majani. Koroga kisha funika kidogo viive vizuri -takribani dakika 3.
 • Bilinganya likishaiva, toa kwenye oven, acha lipoe vizuri kisha menya ngozi. Weka nyama ya ndani ya bilinganya kwenye bakuli safi, kisha ponda vizuri hadi uwe uji mzito. Changanya kwenye sufuria yenye sauce ya mboga za majani. Koroga pamoja kisha acha iive kwa dakika 5.
 • Mapishi haya yametumia samaki wa kukaanga aliyepikwa kama ilivyoelekezwa hapa. Changanya kipande cha samaki kisha acha achemke kwa dakika 5 zaidi, epua mboga na weka pembeni.
 • Unaweza kula mboga hii na chakula chochote upendacho – ugali, wali, ndizi, couscous au unachopendelea. Jirambe kwa raha zako.

ugali-samaki-bilinganya-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Mapishi ya kabeji
dakika 12
Walaji: 4

Samaki wa mchuzi wa nazi
dakika 15
Walaji: 5

Mapishi ya spinach
dakika 18
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.