Samaki mchuzi kwa mapishi tofauti

Mapishi haya yanaweza kupika samaki aina yeyote – mbichi, aliyekaushwa au aliyekaangwa. Ni maalumu kwa kubadilisha ladha ya mapishi kutokana na chaguo la samaki wako. Unaweza kupata njia tofauti za kuongeza ujuzi wa kuandaa samaki wako.

Mahitaji

 • Samaki 2 (Tunatumia samaki wabichi)
 • Vitunguu maji
 • Vitunguu saumu
 • Nyanya
 • Mafuta
 • Ndimu
 • Chumvi
 • Carrots
 • Tangawizi
 • Pilipili hoho

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Andaa vitunguu saumu, tangawizi na ndimu. Tenga kitunguu saumu kwenye sehemu mbili.
 • Osha na kisha marinate samaki wako – weka tangawizi, vitunguu saumu, ndimu na chumvi.
 • Acha samaki akae kiasi – ikiwezekana kwenye jokofu – ili viungo viingie vizuri.
 • Menya vitunguu, nyanya, pilipili hoho na karoti na kisha kata vipande vidogo.
 • Weka mafuta kwenye kikaangio kilicho jikoni. Subiria yapate moto vizuri.
 • Weka samaki na ukaange hadi aive vizuri. Ukimaliza weka samaki pembeni.
 • Bandika sufuria, weka mafuta uliyokaangia samaki. Subiria yapate moto vizuri kisha weka vitunguu na uvikaange mpaka viwe vya kahawia.
 • Weka pilipili hoho na koroga mchanganyiko.
 • Weka vitunguu saumu huku ukiendelea kukoroga kuzuia visigande kwenye sufuria.
 • Weka karoti na endela kukoroga
 • Weka nyanya kisha funika kwa muda wa dakika 5. Hakikisha kuwa moto si mkali sana, bali uwe wa wastani.
 • Kamulia ndimu kwenye mchanganyiko na weka chumvi kisha koroga kiasi.
 • Weka samaki na ongeza maji kiasi (usifanye hapo kwa mama ntilie mchuzi maji tu, hapo nyumbani jaribu kuandaa mchuzi mzito)
 • Acha mboga ichemeke. Maji yakikaukia mchuzi wako utakua tayari na unaweza kula na chakula chochote.

MAPISHI YAPENDWAYO

Viazi na meatballs za nazi
dakika 20
Walaji: 4

Tambi za mayai
dakika 15
Walaji: 4

Biryani ya nyama
dakika 45
Walaji: 6

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.