Samaki wa kukaanga

Kuna wakati unahitaji kuandaa kitu rahisi, kitamu na kinachotumia muda mfupi. Basi huyu samaki ndio chaguo mahsusi kwa wakati kama huo. Ni samaki mwenye viungo vichache lakini mtamu sana. Ni vizuri kwa kumla kwa ugali, maana huyu samaki akiiva vizuri anaweza kuliwa hadi miba.

Mahitaji

Haya mahitaji ni kwa samaki 2 tu. Ila kama una samaki wanaozidi wawili ongeza vipimo vya mahitaji kulingana na idadi ya samaki.

 • Samaki 2 (Andaa kwa idadi inayotosha kwa mahitaji yako)
 • Pilipili manga ya unga kijiko 1 kidogo
 • Mafuta ya kupikia
 • Kiungo chenye ladha (Binafsi huwa natumia maggi cube, lakini unaweza kuwa na kiungo chochote cha chakula, mfano royco au knorr ambazo huwa na ladha tofauti – ng’ombe, kuku, samaki n.k viko madukani)
 • Limao au ndimu 1 ( unaweza pia kutumia vinegar kijiko 1 kikubwa kwa kila samaki)
 • Chumvi
 • Kitunguu saumu 1, menya, kisha ponda vizuri.
 • Tangawizi 1, menya kisha ponda

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Andaa samaki - osha, kwangua magamba kisha kata vipande. Kama una chombo kinachotosha kupika samaki mzima na akaiva vizuri huna ulazima wa kukata vipande.
 • Kamulia limao (au ndimu au vinegar – ni chaguo lako). Paka vizuri limao ndani na nje ya samaki.
 • Nyunyuzia chumvi na pilipili manga. Paka vitunguu saumu na tangawizi. Weka viungo vingine upendavyo kwenye samaki. Hakikisha viungo vimepakwa vizuri nje na ndani ya samaki. Hifadhi samaki pembeni au kwenye jokofu kwa muda ili viungo viingie vizuri, takribani dakika 15. Ila kama huna muda unaweza pia kuandaa moja kwa moja.
 • Bandika kikaango (frying pan) na mafuta jikoni. Mafuta yakipata moto weka samaki. Kaanga vizuri upande mmoja, kisha geuza upande wa pili. Toa samaki akiwa tayari.
 • Jirambe samaki na chakula upendacho.
 • Unaweza kula samaki hawa na vyakula vingi – ugali, wali, ndizi, viazi, mihogo n.k

misosi-samaki-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Supu ya kuku
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.