Samaki wa kukaanga aliyechovywa

Samaki ni chakula nikipendacho sana. Huwa napenda kuandaa samaki tofauti kwa mapishi yanayonivutia. Hii ni aina mojawapo ya mapishi ya samaki wa kukaanga nnayoyapenda. Samaki huyu unaanza kutamani harufu yake wakati wa kumkaanga hadi unapomalizia kula mwiba wa mwisho. Ni kazi kwako kujiramba na kufaidia maisha.

Mahitaji

 • Samaki 2, andaa kwa mahitaji yako
 • Kitunguu saumu
 • Limao
 • Mafuta ya kula
 • Pilipili manga
 • Chumvi
 • Tangawizi ya unga kijiko 1 kidogo

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Huyu samaki ni rahisi kuandaa na mtamu kumla. Anapikwa kwa muda mfupi na utamu wake hauna maelezo.

misosi-fried-fish

 • Andaa samaki – toa magamba, safisha vizuri kisha weka pembeni. Paka chumvi vizuri kwenye samaki.
 • Tengeneza marinade - changanya viungo vyote pamoja kasoro limao. Kisha changanya limao na koroga vizuri.
 • Paka marinade kwenye samaki, hakikisha imeenea vizuri. Acha samaki akae kwa muda wa dakika 10 hadi 15 ili iingie vizuri.
 • Weka kikaango jikoni, acha kipate moto vizuri. Weka mafuta ya kula. Acha yapate moto vizuri sana. Weka samaki, acha aive upande mmoja kisha geuza upande mwingine.
 • Samaki akishaiva, epua na weka pembeni. Jiandae kula samaki mwenye ladha tamu ili kupendezesha siku yako.

misosi-fried-fish2


MAPISHI YAPENDWAYO

Chicken Curry
dakika 30
Walaji: 3

Cornbread yenye korosho
dakika 40
Walaji: 6

Bata wa mchuzi wenye Bizari
dakika 40
Walaji: 6

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.