Samaki wa kuoka aliyetiwa limao

Tunapika samaki wa kuoka kwenye oven bila viungo vingi. Mapishi haya yanatumia chumvi na limao tu. Ni chakula rahisi kuandaa na pia matokeo yake ni mazuri sana. Ni vizuri kujaribu, onja na ujue ladha ya maisha

Mahitaji

 • Samaki
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • Limao
 • Olive Oil
 • Ndizi mzuzu 2
 • Pilipili manga (Mahsusi kwa ndizi mzuzu)
 • Cube maggie (Mahsusi kwa ndizi mzuzu tu)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Leo tunaenda kuandaa samaki na ndizi za kuoka ambaye ataonekana kama hivi tukimaliza

20141217_221113

 • Andaa samaki – toa utumbo, magamba na osha vizuri. Kisha weka kwenye chombo kikavu pembeni. Ni vizuri kama utatumia bakuli la kuokea kwenye oven ili iwe rahisi.
 • Nyunyiza limao vizuri juu ya samaki – nje na ndani kwa uwiano ulio sawa ili samaki apate ladha nzuri ya limao au ndimu.
 • Nyunyiza chumvi vizuri nje na ndani

20141217_202157

 • Kata vitunguu maji, weka pamoja na samaki. Ni vizuri kama utamuweka samaki juu ya vitunguu ili iwe rahisi majimaji yakichuja yanaangukia kwenye vitunguu.

20141217_203239

 • Menya ndizi mzuzu na kisha kata vipande vidogo wastani. Nyunyiza pilipili manga na cube maggie kiasi. Changanya vizuri.

20141217_203645

20141217_203859

 • Weka ndizi kwenye chombo chenye samaki.
 • Nyunziza mafuta ya olive kiasi, kisha paka vizuri kwenye vitunguu pamoja na samaki. Mafuta ni muhimu ili kusaidia samaki aive vizuri bila kuungua. Hakikisha humwagii mafuta mengi.

20141217_210749

 • Hifadhi samaki vizuri sehemu ili viungo vipate kuingia. Inaweza kuwa takribani dakika 45 hadi saa 1
 • Baada ya saa 1, washa oven kwenye nyuzi 250°C na acha lipate moto kwa takribani dakika 10.
 • Weka samaki kwenye oven na tega muda dakika 45.

20141217_220122

 • Mara kwa mara hakikisha samaki haungui, mgeuze inapolazimu ili asiungue.
 • Baada ya muda toa samaki na yuko tayari kuliwa

20141217_221113

20141217_221226


MAPISHI YAPENDWAYO

Dagaa wenye curry sauce
dakika 25
Walaji: 2

Sweet & Sour Chicken
dakika 45
Walaji: 2

Cream cheese pound cake
dakika 80
Walaji: 6

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.