Samaki wa kuoka kwa sauce ya bizari

Kama una ulimi unaojua vitamu na vyenye afya, basi huyu ndio samaki wa kula. Unapata ladha ya viungo tofauti vyenye kukupa afya, lakini pia unapata virutubisho muhimu toka kwenye samaki. Samaki wa kuoka anaweza kuliwa kila kitu, ikiwezekana hata miba kama imeiva vizuri :) . Kazi kwako

Mahitaji

 • Samaki 1
 • Limao 1 (tengeneza juice ya kutosha ili kuloweka samaki vizuri)
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Bizari ya njano kijiko 1 kidogo
 • Bizari nyembamba kijiko 1 kidogo
 • Kitunguu saumu cha unga kijiko 1 kidogo
 • Kijiko 1 kikubwa cha mafuta ya kula (nimetumia olive oil)
 • Tandoori (Si lazima kutumia kama hutakuwa nayo) kijiko 1 kidogo

Mahitaji ya ziada

Binafsi nilipenda kuandaa huyu samaki na viazi, ili nipate mlo kamili wa kuoka. Hivyo nikaongeza vitu vichache ili kuupa mlo mvuto na ladha zaidi.

 • Viazi mbatata 4
 • Kitunguu 1
 • Pilipili hoho 1
 • Karoti 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Mie napenda sana samaki. Huwa napenda kuandaa samaki kwa mapishi tofauti kwa kutumia viungo tofauti ili kuonja ladha mbalimbali. Mara nyingi huwa napendelea samaki wa kuoka, maana huwa anaiva vizuri sana, pia hakuna mafuta mengi na anakuwa na ladha tamu tofauti na kukaanga, haya ni maoni yangu tu. Pishi hili la samaki ndio kama hivyo, tamu na lenye ladha nzuri, na samaki alikuwa mtamu kama anavyoonekana.

Ukimaliza kuandaa samaki atakuwa anaonekana kama hivi.

misosi-samaki-viazi

 • Andaa samaki. Toa magamba, osha vizuri kisha weka kwenye chombo kikavu. Mchanje kidogo pembeni, hii itaruhusu sauce kuingia vizuri kwenye samaki.
 • Changanya pamoja viungo kwa kutengeneza sauce (marinade) - bizari (wengine huita binzari) ya njano, bizari nyembamba, mafuta, tandoori (kama unatumia), chumvi na juisi ya limao. Changanya hadi kila kitu kichanganyike vizuri. Hakikisha sauce isiwe nzito sana ili uweze kupaka kwenye samaki.
 • Paka sauce (marinade) vizuri pande zote mbili za samaki. Hakikisha sauce imeenea vizuri ndani na nje ya samaki. Weka samaki pembeni.
 • Washa oven kwenye nyuzijoto 350°F (180°C). Acha ipate moto. Au unaweza pia kuchoma kwenye jiko la mkaa.
 • Mie nimeandaa huyu samaki pamoja na viazi, hivyo unaweza kuandaa viazi kwa kuvikata vyembamba kiasi pamoja na kitunguu, karoti na pilipili hoho.
 • Weka samaki kwenye chombo cha kuokea (kama unatumia oven ni vizuri ukitumia waya wa kuokea ili samaki achuje maji maji vizuri). Mie niliweka viazi na mboga mboga chini ya samaki ili viive kwa pamoja, pia mchuzi uliotoka kwenye samaki umeleta ladha nzuri kwenye mboga mboga. Tega dakika 35 hadi 40 ili samaki apate kuiva.
 • Baada ya samaki kuiva, toa na hakikisha yuko vizuri. Kama bado hajaiva vizuri acha kwenye oven kwa dakika nyingine 5 hadi 10. Akishaiva andaa chakua na jirambe kwa raha zako.
 • Samaki huyu unaweza kumla na chakula chochote kile -  ugali, wali, mihogo, au viazi kama nilivyokula mimi.

misosi-samaki-viazi


MAPISHI YAPENDWAYO

Chocolate crinkles
dakika 10
Walaji: 5

Viazi lishe, karoti na maziwa
dakika 20
Walaji: 1

Wali wa viungo
dakika 20
Walaji: 4

Tambi za sausage na kuku
dakika 45
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.