Samaki wa kuoka kwa viungo mchanganyiko

Tunapika samaki wa kuoka kwenye oven akiwa amechanganyika na ndizi mzuzu. Mapishi haya yanatumia viungo mbalimbali ili kumfanya samaki awe laini, wa kuvutia na ladha nzuri kwa kumla. Mie hufurahia chakula hiki maana hunipa matokeo bora kwa muda wangu nnaotumia katika kuandaa. Karibu ujumuike nasi katika kuandaa chakula bora.

Mahitaji

 • Samaki 1
 • Kitunguu saumu
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • Limao au ndimu 1
 • Pilipili manga
 • Tangawizi 1
 • Vitunguu maji 2
 • Ndizi mzuzu 2
 • Olive oil

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Tunaandaa samaki wa kuoka kwenye oven ambaye akimalizika atakuwa kama hivi:

20141210_194820

 • Andaa samaki – toa utumbo, magamba na osha vizuri. Kisha weka kwenye chombo kikavu pembeni. Ni vizuri na rahisi kama utatumia bakuli la kuokea kwenye oven.

20141210_180426

 • Nyunyiza limao vizuri juu ya samaki – nje na ndani kwa uwiano ulio sawa ili samaki apate ladha nzuri ya limao au ndimu.
 • Nyunyiza chumvi vizuri nje na ndani
 • Ponda kitunguu saumu (au kama una kitunguu saumu cha unga) kisha paka juu ya samaki vizuri, nje kwa ndani.
 • Nyunyizia pilipili manga ya unga juu yake na mpake kwa ndani pia. Hakikisha unaweka hii kama unakula pilipili, kama hutumii pilipili hii hatua si lazima.
 • Weka tangawizi kwenye samaki. Paka vizuri kwa nje na  ndani.
 • Menya ndizi mzuzu na kisha kata vipande na weka kwenye bakuli lenye samaki.
 • Kata vitunguu maji, weka pamoja na samaki. Ni vizuri kama utamuweka samaki juu ya vitunguu ili iwe rahisi majimaji yakichuja yanaangukia kwenye vitunguu.
 • Nyunziza mafuta ya olive kiasi, kisha paka vizuri kwenye vitunguu pamoja na samaki. Mafuta ni muhimu ili kusaidia samaki aive vizuri bila kuungua. Hakikisha humwagii mafuta mengi.

20141210_181905

 • Hifadhi samaki vizuri sehemu ili viungo vipate kuingia. Inaweza kuwa takribani dakika 45 hadi saa 1
 • Baada ya saa 1, washa oven kwenye nyuzi 250°C na acha lipate moto kwa takribani dakika 10.
 • Weka samaki kwenye oven na tega muda dakika 45.

20141210_193631

 • Mara kwa mara hakikisha samaki haungui, mgeuze inapolazimu ili asiungue.
 • Baada ya samaki kuiva, tenga chakula tayari kuliwa. Mlo mwema.

20141210_194245

20141210_194829

20141210_194751

Chakula chema, ujirambe na ladha ya maisha 


MAPISHI YAPENDWAYO

Macaroni ya cheese
dakika 20
Walaji: 3

Peanut butter cookies
dakika 10
Walaji: 5

Chocolate crinkles
dakika 10
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.