Samaki wa kupaka

Samaki ni chakula kitamu, lakini samaki wa kupaka ni mwisho wa maelezo. Akipikwa kwa kutumia viungo bora, vyenye mchanganyiko mzuri, unapata matokeo yanayokupa raha kula chakula. Chakula ni kitu muhimu sana, hivyo lazima ufurahie kuandaa hadi kula. Huyu samaki wa kupaka ni mfano mzuri wa chakula kinachopendeza kuanzia kuandaa hadi kuliwa.

Mahitaji

 • Samaki 2
 • Tui zito la nazi kikombe 1
 • Kitunguu maji 1
 • Karoti 2
 • Kitunguu swaumu 1
 • Iliki 1
 • Pilipili mbichi 1 (kama unatumia pilipili)
 • Nyanya 3
 • Ndimu 1
 • Chumvi Kijiko 1 kikubwa
 • Tandoori powder vijiko 2 vikubwa
 • Mafuta ya kula, tumia mafuta ya zaituni – olive oil

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kuongea au kupunguza viungo kwenye haya mapishi kama unavyopendelea. Hakikisha unaandaa huyu samaki kutokana na mahitaji yako.

misosi-samaki-kupaka-main

 • Andaa viungo – menya nyanya, kitunguu saumu, karoti, kitunguu maji, karoti, iliki. Changanya kwa pamoja. Weka viungo vikavu vilivyobaki, kasoro pilipili. Saga kwa pamoja upate uji mzito.
 • Osha samaki, pasua mistari juu ya samaki ili viungo viingie vizuri kwenye samaki. Nyunyizia ndimu (au limao, au siki) na chumvi nje na ndani ya samaki. Paka vizuri ndani na nje ya samaki. Nyunyizia pilipili juu yake. Acha samaki wakae kwa dakika kama 15 hadi 20 ili viungo vipate kuingia. 
 • Washa oven kwenye nyuzijoto 190°C (370°F), acha ipate moto kwa muda wa dakika 7 hadi 10. Paka mafuta ya kula juu ya samaki ili kumfanya aive vizuri bila kuungua. Hakikisha unapaka mafuta kiasi tu, usilundike. Tumia mafuta yenye afya kama olive oil ili uboreshe afya. Weka samaki kwenye oven. Acha aive vizuri kwa muda wa dakika 40 hadi 50. Hakikisha joto linagawanyika vizuri ndani ya oven. Unaweza pia kutumia jiko la mkaa kuoka huyu samaki. Kama unatumia jiko la mkaa, weka moto mdogo sana kisha mbanike ili aweze kuiva kwa joto kiasi, ili asiungue nje na kutoiva vizuri ndani. Geuza mara kwa mara ili samaki aive vizuri pande zote.
 • Wakati samaki anaokwa, andaa mchuzi wa kuchovya samaki. Bandika chungu au sufuria jikoni, kikipata moto weka tui la nazi. Koroga tui huku ukiwa unaongeza viungo ulivyosaga hapo awali. Ongeza ndimu na chumvi. Angalia usizidishe chumvi maana samaki ana chumvi pia. Usiache kukoroga ili kufanya tui kuwa laini kwa matokeo mazuri zaidi. Koroga mchanganyiko wa tui hadi likauke na kuwa kitu kimoja na viungo vyake.
 • Samaki akishaiva, toa hifadhi pembeni. Kwenye bakuli safi, paka rojo ya nazi uliyoandaa kiasi. Weka samaki juu yake. Endelea kupaka rojo juu ya samaki. Hakikisha rojo imeenea vizuri ndani na nje ya samaki. Geuza samaki upande wa pili, paka vizuri hadi rojo ienee vizuri.
 • Weka samaki kwenye moto, kwenye oven au kwenye jiko la mkaa. Acha samaki aive kwa muda wa dakika 15 hadi 20 ili viungo viingie vizuri.
 • Tenga mboga na ujirambe na ubora wake.

Unaweza kula mboga hii na wali, ugali, maandazi, chapati, au ukachanganya na mboga za majani.

misosi-samaki-kupaka-main0


MAPISHI YAPENDWAYO

Maandazi ya Mayai na Maziwa
dakika 20
Walaji: 4

Samaki wa kupaka
dakika 25
Walaji: 2

Tambi za hiliki na sukari
dakika 8
Walaji: 2

Ndizi za kuunga na nazi
dakika 20
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.