Samaki wa kwenye foil mwenye ndimu

Samaki ni chakula kizuri sana, hasa akipikwa kwa staili kama hii ambapo anaiva kutokana na juisi yake mwenyewe ndani ya foil paper. Uzuri wa mapishi haya ni kuwa unapata mchuzi ambao unaweza kuuongeza kwenye mboga tofauti ilikupata ladha ya limao na viungo vya samaki.

Mahitaji

 • Samaki 1
 • Ndimu 1
 • Pilipili hoho
 • Kitunguu 1 au (2 kama ni vidogo)
 • Chumvi
 • Maggi cube (Hii siyo lazima, mie nilitumia maana nilitaka kuongeza ladha tu)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Ukimaliza kuandaa samaki atakuwa anaonekana kama hivi

main

 • Washa oven kwenye nyuzijoto 180°C (350°F) ili ipate moto wakati unaandaa samaki.
 • Andaa samaki. Toa magamba, osha vizuri kisha weka kwenye chombo kikavu. Mkate kwa alama ya X vizuri pande zote mbili ili apate kuiva vizuri kwa ndani. Nyunyuzia chumvi juu ya samaki pande zote mbili.

20150209_183045

 • Andaa kitunguu, karoti, na pilipili hoho kwa kuzitaka kwenye vipande virefu wastani.
 • Andaa foil paper, tandaza vitunguu vizuri kwa chini. Weka samaki juu yake. Malizia kwa kuweka mboga mboga pembeni ya samaki pia.

20150209_185415

 • Kata limao kwenye vipande vyembamba, tandaza juu ya samaki vizuri kwa urefu.

20150209_185651

 • Funga foil paper yako vizuri. Weka kwenye oven na tega muda wa saa 1 au dakika 60.
 • Baada ya samaki kuiva, toa na hakikisha yuko vizuri. Kama unapenda samaki aliyemalizika kupikwa hivi unaweza kumla moja kwa moja, maana ni mtamu sana tu. Mie nilikuwa nataka awe mkavu kidogo, hivyo nikaongeza hatua moja.

20150209_202146

 • Mwagia unga wa maggi cube juu ya upande wa samaki ulio juu. Usifunike foil paper, rudisha kwenye oven kwa dakika 5 nyingine, samaki ataiva vizuri na kuanza kukauka na kuwa mgumu kiasi. Mie napenda akiwa hivi, ndio maana nikaendelea kumuweka kwenye moto kwa muda mrefu kiasi.
 • Samaki huyu unaweza kumla na chakula chochote kile -  ugali, wali, mihogo, au viazi. Jirambe na samaki wa kuoka.

20150209_210119

20150209_210533

fish


Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.