Samaki wa mchuzi wa nazi

Samaki ni chakula muhimu sana,mana kutoka kwa samaki tunafaidi vitu muhimu sana mana tunapata virutubisho vingi sana kama madini ya chuma,vitamin D. Pia husaidia kama dawa.

Mahitaji

 • Nyanya
 • Pilipili hoho
 • Vitunguu maji
 • Vitunguuswaumu
 • Carrots
 • Ndimu
 • Nazi (tui zito)
 • Chumvi
 • Samaki
 • Tangawizi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Andaa viungo – tangawizi, ndimu, vitunguu saumu – menya, kata na ponda kama inawezekana.
 • Osha samaki vizuri kisha mloweke kwenye viungo (chaganya tangawizi,ndimu,vitunguu saumu na chumvi) kwa muda wa saa moja.
 • Andaa viungo vyako mbadala – nyanya,vitunguu,karoti, na pilipili hoho. Tengeneza tui zito la nazi na hifadhi pembeni.
 • Bandika kikaangio, au sufuria jikoni, weka mafuta ya kula na acha yapate moto.
 • Weka samaki. Kaanga samaki ila hakikisha asikauke sana.
 • Fanya hivyo kwa samaki wote waliobaki.
 • Bandika sufuria jikoni weka mafuta kiasi – unaweza pia kutumia uliyokaangia samaki
 • Mafuta yakipata moto, weka vitunguu maji kisha koroga hadi kibadilike rangi kiwe rangi ya udongo.
 • Weka kitunguu saumu kisha koroga kidogo kama dakika 1
 • Weka pilipili hoho na karoti. Koroga kiasi, kwa takribani dakika 2.
 • Weka nyanya, koroga kiasi ili zichanganyike vizuri. Funika na mfuniko na acha ziive kwa mvuke.
 • Nyanya zikiiva, weka tui zito liache lichemke kama dakika 10.Mchuzi ukiwa mzito weka samaki na koroga mpaka samaki achanganyikane na viungo vizuri. Acha jikoni kwa dakika takribani 3 nakisha ipua.
 • Hapo msosi utakua tayari

MAPISHI YAPENDWAYO

Mapishi ya nundu
dakika 15
Walaji: 3

Kuku wa kuoka
dakika 120
Walaji: 5

Nguru wa kuchoma
dakika 40
Walaji: 2

Chilly beef
dakika 60
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.