Samaki wa mvuke kwa bilinganya na sauce ya kitunguu saumu

Chakula hiki ni kinavutia na kitamu sana, kitakufanya ufurahie siku yako vizuri. Pia mtu ambaye yupo kwenye diet anaweza kula vizuri mana chakula kimepikwa kiafya zaidi .

Mahitaji

 • Samaki 1, unaweza kumkata vipande au apikwe mzima
 • Bilinganya 2
 • Soy sauce kijiko 1 kikubwa 
 • Mafuta vijiko 2 vya chakula, binafsi nimetumia olive oil
 • Kitunguu saumu ½ kijiko kidogo
 • Tangawizi ½ kijiko kidogo
 • Mboga za majani, nimetumia greenbeans na kolimaua
 • Vitunguu maji 2
 • Pilipili hoho nusu
 • Karoti 1
 • Cayenne pepper kiasi
 • Chumvi kiasi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Chakula hiki kinapikwa kwa awamu mbili tofauti, lakini baada ya muda mfupi utakuwa unajiramba.

misosi-fish-mvuke-2

1. Kuandaa mboga za majani 

 • Osha bilinganya, kata vipande vidogo kisha loweka kwenye maji yenye chumvi ili zisibadilike rangi.
 • Menya kisha kata vipande – kitunguu saumu, pilipili hoho, vitunguu maji na karoti
 • Bandika sufuria, weka maji, ongeza mafuta na chumvi kwenye maji. Acha maji yachemka kisha weka bilinganya. Toa baada ya dakika 5.
 • Bandika kikaango jikoni. Weka mafuta, yakipata moto weka kitunguu saumu na tangawizi. Koroga vizuri kwa dakika 3. Weka kitunguu maji, karoti na pilipili hoho. Koroga vizuri, nyunyizia cayenne pepper.
 • Weka mboga mboga, soy sauce na bilinganya. Pika kwa dakika 7, epua kisha jirambe 

2. Kuandaa kipande cha samaki

 • Andaa samaki kwa kutoa magamba kisha osha vizuri. Pasua mistari kwenye pande za samaki. Paka viungo vya samaki masala, chumvi, cayenne pepper na nyunyizia ndimu. Pika samaki kwa kutumia mvuke. Acha hadi aive vizuri.
 • Tenga samaki na mboga za majani upate kujiramba.

misosi-samaki-mvuke-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Ndizi mzuzu zilizoiva
dakika 13
Walaji: 2

kisamvu cha nazi
dakika 30
Walaji: 4

Mapishi ya nyama ya kusaga
dakika 30
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.