Samaki wa ngano na tangawizi

Raha ya samaki aliwe akiwa bado wa moto. Lakini huyu pia ana vionjo vya ziada. Viungo alivyowekewa anakuwa mtamu zaidi. Anaweza kuliwa kwa ugali, wali hata kama kitafunwa kawaida na chachandu pembeni. Jirambe na pishi hili murua.

Mahitaji

 • Vipande 2 vya samaki (Mimi nimetumia Salmon fish)
 • Ngano kidogo (Kidogo sana maana ni ya kunyunyizia tu)
 • Tangawizi ya unga kijiko 1 cha chai
 • Kitunguu saumu punje 4 zilizopondwa, au kijiko 1 cha chai kama ni ya unga
 • Mafuta ya kula (Mie nimetumia olive oil)
 • Chumvi kijiko 1 cha chai

 

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Leo tunatayarisha samaki wa ngano, tangawizi pamoja na kitunguu saumu

a20150117_150732

 • Osha samaki na kisha weka kwenye chombo kikavu

20150117_141546

 • Nyunyizia chumvi kidogo. Paka vizuri hadi samaki aendee.
 • Paka kitunguu saumu juu ya samaki.
 • Mwagia tangawizi ya unga (Au kama umeponda, paka maji maji juu ya samaki)
 • Nyunyizia kidogo kidogo juu ya samaki unga wa ngano. Kisha geuza samaki ilia pate kuenea unga pande zote.
 • Acha samaki akae kwa dakika 5 hadi 10 ili viungo vipate kuingia vizuri.

20150117_142457

 • Bandika kikaango (frying pan) jikoni na weka mafuta. Acha yapate moto kwa muda.
 • Weka samaki na kaanga. Geuza wakishaiva ili waive upande mwingine. Hakikisha hugeuzi geuzi samaki akiwa kwenye mafuta maana kama hajaiva vizuri anaharibika sababu bado anakuwa ameganda kwenye kikaango.

20150117_143546

 • Unaweza kula samaki huyu na ugali, wali au chakula chochote unachopendelea. 
 • Jirambe na ladha ya maisha

20150117_150712


MAPISHI YAPENDWAYO

Chocolate Fondant Pudding
dakika 20
Walaji: 8

Koni za asali
dakika 25
Walaji: 10

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.