Samaki wa mchuzi wa nazi

Samaki ni chanzo kikubwa cha protini na mafuta yasiyojaa mwilini. Vyakula vya baharini kuwa ni afya njema maana havina mafuta yanayoharibu mwili na huwa na virutubisho vingi asilia. Hii mboga iliyochananywa na mboga za majani ni chakula muafaka cha kukupa virutubisho, ladha na hamu ya kula zaidi kwa afya bora.

Mahitaji

 • Samaki vipande 4
 • Vitunguu maji 3
 • Karoti kubwa 1
 • Pilipili hoho 1
 • Bizari nyembamba nusu kijiko cha chai
 • Mafuta vijiko vya chai 3
 • Chumvi
 • Nazi iliyokomaa vizuri 1
 • Ndimu au limao 1
 • Kitunguu saumu 1
 • Nyanya kubwa zilizoiva vizuri 4
 • Bamia 5
 • Nyanya chungu 4
 • Nyanya ya kopo kijiko 1 kikubwa

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Mapishi haya yanatumia samaki aliyekwishakaangwa. Unaweza kuandaa samaki kwa kufuata maelezo yaliyomo kwenye mapishi haya ya samaki.

 • Andaa vipande vya samaki vilivyokaangwa vizuri weka pembeni.
 • Bandika sufuri bandika jikoni, weka mafuta ya kula. Mafuta yakipata moto weka kitunguu maji, kaanga hadi kiive vizuri.
 • Weka nyanya chungu na bamia. Koroga kisha weka nyanya, koroga na punguza moto. Hakikisha nyanya zimeiva na zimejitenga na mafuta kisha weka nyanya ya kopo. Pika kwa takribani dakika 3.
 • Weka pilipili hoho na karoti, koroga kama dakika 2 kisha weka tui jepesi na chumvi. Acha tui lichemke kisha weka samaki. Koroga taratibu kama dakika 5. Weka tui zito huku ukikoroga hadi tui lichemke. Weka bizari nyembamba na kitunguu saumu, koroga. Acha mboga ichemke kama dakika 5, epua.
 • Unaweza kula mboga hii na vyakula tofauti – ugali, wali, ndizi, mihogo, maandazi, mkate na vyakula tofauti. Jirambe na ladha ya maisha.

fishmisosi


MAPISHI YAPENDWAYO

Keki ya chocolate
dakika 55
Walaji: 4

Lemonade ya tangawizi
dakika 70
Walaji: 6

Kabeji yenye royco
dakika 10
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.