Samaki wenye sauce ya pilipili

Mboga hii ya samaki ni nzuri kwa wale wanaopenda kula mboga yenye pilipili na vionjo tofauti vya viungo.Unaweza kutumia samaki wadogo au vipande vya samaki wakubwa na kuandaa mboga hii. Kutokana na samaki utakaotumia matokeo yatatofautiana, lakini ubora wa mboga uko pale pale.

Mahitaji

 • Samaki 6 (wadogo) au vipande 6 (kama ni wakubwa)
 • Tangawizi ya unga kijiko 1
 • Mafuta ya kula, nimetumia mafuta ya zaituni (Olive)
 • Kitunguu maji 1, kata vipande
 • Kitunguu saumu punje 5, ponda
 • Pilipili hoho 2, mie nimechanganya za rangi tofauti
 • Chumvi kijiko 1
 • Pilipili manga ya unga kijiko 1
 • Pilipili 2  (cayenne pepper)
 • Nyanya maji 2, menya kisha kata vipande au unaweza kusaga
 • Nyanya ya kopo vijiko 2

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kutumia samaki wadogo au vipande vya samaki wakubwa na kuandaa mboga hii.

Kuandaa samaki

 • Andaa samaki – kwangua magamba, toa utumbo kisha osha vizuri. Hifadhi pembeni. Rudia hii hatua hadi samaki wote waishe. Ukimaliza kuandaa nyunyizia chumvi, tangawizi na juu ya samaki. Paka tangawizi kiasi na kisha kamulia limao na changanya vizuri. Acha samaki wakae kwa muda wa dakika 15 hadi 20 ili limao liingie vizuri.
 • Bandika kikaango jikoni, acha kipate moto vizuri. Weka mafuta ya kula, acha yapate moto vizuri sana. Mafuta yakipata moto weka samaki, hakikisha usilundike ili waive vizuri.
 • Geuza samaki ili waive vizuri pande zote. Samaki wakishaiva toa na hifadhi pembeni, kwenye karatasi inayonyonya mafuta (paper towel). Rudia hatua hii hadi samaki wote waive.

Kuandaa sauce

Kwenye mboga hii unaweza kuongeza viungo unavyopendelea ili kupata mboga bora na tamu.

 • Osha kisha kata pilipili hoho, kitunguu saumu, kitunguu maji na pilipili za kawaida. Hifadhi kwenye chombo safi pembeni.
 • Bandika kikaango au sufuria jikoni. Kikipata moto weka mafuta ya kula vijiko 2, acha yapate moto vizuri kisha weka kitunguu maji na kitunguu saumu. Funika ili vipate kulainika na kuchuja maji ili wive laini na kuwa rangi ya kahawia.
 • Weka nyanya, koroga pamoja. Funika na acha nyanya ziive vizuri kwa dakika 5 hadi 7 kisha weka pilipili hoho, koroga kiasi. Weka pilipili za kawaida, koroga zaidi. Funika sufuria vizuri, acha vichemke pamoja kwa dakika 5.
 • Weka samaki, kuwa muangalifu usikoroge sana maana samaki wataharibika. Acha mboga ichemke kwa dakika 5 hadi 7. Epua na kisha andaa pamoja na wali, ugali au chakula chochote upendacho.

samaki-misosi-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Vitumbua vya mayai
dakika 10
Walaji: 6

Brown rice, maziwa na karoti
dakika 60
Walaji: 1

Chicken Curry
dakika 30
Walaji: 3

Cornbread yenye korosho
dakika 40
Walaji: 6

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.