Sambusa za limao na asali

Hii ni aina nyingine ya kuandaa sambusa tamu zenye asali zilizookwa kwenye oven. Sambusa hizi zina cheese na mayai, unaweza kutumia mahitaji tofauti kutokana na unavyopendelea na ukapata matokeo mazuri kabisa. Ni sambusa rahisi kuandaa lakini ubora wake uko vizuri sana kwa kuleta ladha tamu kwa wale walaji.

Mahitaji

 • Ricotta cheese gramu 250
 • Asali gramu 100
 • Sukari gramu 50
 • Limao 1
 • Mayai 2
 • Manda
 • Siagi au mafuta ya kula vijiko 2
 • Unga wa ngano vijiko 4 vya chakula au ute wa yai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuwa huru kuongeza au kupunguza mahitaji kutokana na unavyopendelea.

 • Washa oven kwenye nyuzijoto 180°C (356°F), acha ipate moto vizuri.
 • Andaa lemon zest – Osha kisha kwangua ganda la limao ili kupata ngozi iliyo laini. Hifadhi pembeni.
 • Katika bakuli, changanya ricotta, yai, sukari na zest.
 • Koroga unga wa ngano na ute wa yai, hii itakusaidia kufungia sambusa.
 • Kata manda kwenye umbo la pembetatu kisha weka mchanganyiko wa cheese kwenye sambusa. Anza kufunga sambusa vizuri kisha paka ute wa yai na ngano ili kufanya sambusa zifunge vizuri na zisifunguke wakati wa mapishi. Rudia hii hatua hadi umalize kufunga sambusa zote.
 • Kwenye sinia la kuokea kwenye oven, weka karatasi linaloweza kuingia kwenye oven, kisha panga sambusa juu yake. Paka mafuta kiasi juu yake kwa kutumia brush ya chakula, paka pande zote. Mafuta husaidia kuifanya ngozi ya sambusa isiungue wakati wa kuoka.
 • Oka sambusa kwa dakika 25, hadi zibadilike rangi na kuwa rangi ya dhababu.
 • Pasha moto asali – unaweza kutumia microwave (sekunde 30 hadi 60) au jiko la kawaida (inategemea na ukali wa moto). Asali ikishakuwa ya moto paka taratibu juu ya sambusa kwa kutumia brush ya chakula. Rudia zoezi hili kwa sambusa zote ulizokwisha andaa.
 • Unaweza kula sambusa hizi kama kitafunwa, kwa chai, kwa kinywaji baridi au vyovyote unavyopenda.

misosi-sambusa-asali-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Viazi lishe, karoti na maziwa
dakika 20
Walaji: 1

Wali wa viungo
dakika 20
Walaji: 4

Tambi za sausage na kuku
dakika 45
Walaji: 2

Kuku wa kuoka na ndizi mzuzu
dakika 60
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.