Sambusa za mboga za majani

Sambusa ni kitafunwa kizuri kwa chai au chakula chepesi kwa kuzibia njaa. Sambusa hizi zinaandaliwa kwa mboga za majani ni tamu na zenye afya, maana unapata virutubisho vingi na afya zaidi. Unaweza kuandaa sambusa hizi, ukahifadhi kwenye jokofu na kupika wakati unapohitaji kula.

Mahitaji

 • Viazi ulaya vitatu vilivyochemshwa kisha kata vipande vidogo vidogo
 • Njegere zilichemshwa kidogo nusu kikombe
 • Vitunguu 2 kata vipande vidogo
 • Tangawizi nusu
 • Pilipili 2
 • Mustard seed ½ kijiko cha chai
 • Bizari nyembamba  nusu kijiko cha chai
 • Hing kiasi
 • Bizari nusu kijiko cha chai
 • Giligilani iliyosagwa kijiko 1 cha chai
 • Bizari nyembamba iliyosagwa kijiko 1 cha chai
 • Garam masala nusu kijiko cha chai
 • Majani ya curry manne
 • Limao kijiko 1 cha chakula
 • Mafuta kijiko 1 cha chakula
 • Chumvi kwa ladha
 • Karoti 2 katakata
 • Unga wa ngano vijiko 4 vya chakula au ute wa yai
 • Manda

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuwa huru kuongeza au punguza viungo kutokana na unavyopendelea.

 • Kwenye kinu, weka tangawizi, kitunguu saumu na pilipili. Twanga kwa pamoja hadi vilainike kisha hifadhi pembeni.
 • Bandika sufuria au kikaangio jikoni. Weka mafuta, yakipata moto weka mbegu za mustard, bizari nyembamba, hing na majani ya curry. Pika kwa dakika 2 huku ukigeuza mara kwa mara. Weka mchanganyiko wa pilipili kisha pika hadi harufu ya kitunguu saumu na tangawizi ipotee.
 • Weka kitunguu maji, pika kwa dakika 2 hadi 3 kisha weka mboga yoyote ya majani utakayopenda. Mie nimeweka karoti.
 • Weka viazi ulaya, unga wa giligilani, unga wa bizari nyembamba, bizari, garam masala na chumvi.  Changanya vizuri mpaka viazi vichanganyikane na viungo vingine. Punguza moto uwe wa wastani, pika kwa dakika 5 huku ukikoroga taratibu. Weka njegere na limao. Changanya vizuri pika kwa dakika 2. Epua acha mboga zipoe kabisa.
 • Koroga unga wa ngano au ute wa yai, hii itakusaidia kufungia sambusa.
 • Kata manda kwenye umbo la pembetatu kisha weka mboga mboga kiasi. Anza kufunga ila ukifika mwisho paka ute wa yai au unga wa ngano uliokoroga. Inasaidia sambusa zisifunguke wakati wa kupika.
 • Bandika kikaango chenye mafuta jikoni. Mafuta yakipata moto anza kupika sambusa hadi zigeuke rangi na kua kahawia. Epua na hifadhi pembeni. Rudia hii hatua hadi sambusa zote ziive.
 • Tenga sambusa na jirambe.

misosi-sambusa-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Tambi zenye iliki na sukari
dakika 8
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.