Sambusa za nyama

Sambusa za nyama hupendwa na watu wengi mana ni tamu, unaweza kula kwa soda, juice au chai, pia waweza kula zenyewe tu na ukafurahi

Mahitaji

 • Nyama steki kilo 1 ( mi nina mashine ya kusagia kama huna nunua ya kusaga)
 • Vitunguu maji 2
 • Majani ya Giligiliani vifungu 2 
 • Garam masala kijiko 1 cha chai
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • Pilipili manga kikijo 1 cha chakula
 • Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1 cha chai
 • Tangawizi ya Unga kijiko 1 cha chai
 • Karoti 2 kubwa
 • Pilipili hoho 2
 • Unga wa ngano vijiko 4 vya chakula au ute wa yai
 • Manda
 • Butter kijiko kimoja cha chakula

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Bandika nyama weka chumvi, mpaka iive iwe laini. Hamisha supu pembeni ibaki nyama tu.
 • Chukua mashine ya kusagia nyama, weka giligilia kwenye nyama, anza kusaga nyama na giligiliani pamoja, funika weka pembeni.
 • Kata kata vitunguu maji, muundo wa box size ndogo sana, kata karoti na pilipili hoho. Weka pembeni.
 • Chukua frying pan pana, weka butter. Ikianza kuchemka weka vitunguu maji, karoti na pilipili hoho, koroga visiive.
 • Weka kitunguu saumu kilichosagwa, weka pilipili manga na tangawizi koroga vizuri.
 • Weka nyama, koroga vizuri ili ichanganyikane na viungo vingine, weka garam masala koroga dakika 2, epua. Usiifunike
 • Koroga unga wa ngano au ute wa yai, hii itakusaidia kufungia sambusa.
 • Chukua manda, kata kwa umbo la pembetatu. Kisha weka nyama kiasi, anza kufunga ila ukifika mwisho paka ute wa yai au unga wa ngano uliokoroga.
 • Inasaidia sambusa zisifunguke wakati wa kupika.
 • Bandika mafuta yakipata moto anza kupika,mpaka uone sambusa zimegeuka rangi na kua kahawia. Epua anza kujiramba.

MAPISHI YAPENDWAYO

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.