Sandwich ya kienyeji

Hiki huwa nakiita chakula cha kivivu, lakini siku hii nilibadilisha mawazo, maana msosi ulinoga. Nilikuwa na hamu ya kula sandwich lakini sikuwa na muda wa kutoka. Nikaona niandae yangu kawaida, na matokeo yake yakawa haya. Hiki ni chakula unachoweza kuandaa kirahisi nyumbani kwa kutumia muda mchache kabisa, cha muhimu uwe na mahitaji tu. Unaweza kutengeneza sandwich hii na mkate wa aina yeyote ule, si lazima uwe kama ulivyo kwenye picha.

Mahitaji

 • Mayai 2
 • Kitunguu maji 1
 • Nyanya 1 (zisimenywe, maana zinaliwa kama kachumbari)
 • Kitunguu saumu 1 (Kimenywe na kupondwa)
 • Pilipili hoho 2 (napenda zenye rangi tofauti ili kuleta rangi nzuri kwenye chakula)
 • Chumvi
 • Karoti 1 (Menya maganda)
 • Pilipili manga ya unga
 • Mkate (Unaweza pia kutumia mkate wa kutengeneza mwenyewe kama ulivyoelezwa hapa)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Sandwich hii pia inaweza kuliwa kwa kuweka salad, au chochote kingine unachopendelea kula na mkate. Unaweza pia kutumia mkate wa kutengeneza mwenyewe kama ulivyoelezwa hapa. Ni vizuri kujaribu vitu tofauti ili ufahamu ladha tamu ya vyakula.

misosi-sandwich

 • Anza kukaanga mayai – menya kitunguu kizima na karoti nusu, kata vipande vidogo kisha hifadhi kwenye chombo pembeni. Kata pilipili hoho, hifadhi pembeni. Kwenye chombo tofauti, pasua yai, koroga vizuri. Ongeza chumvi, pilipili manga na kitunguu saumu kwenye yai. Koroga pamoja vizuri, hifadhi pembeni.
 • Bandika kikaango jikoni, weka mafuta. Acha yapate moto. Weka kitunguu. Koroga ili kiive na kulainika. Ongeza pilipili hoho na karoti kiasi. Acha ziive kidogo, takribani dakika 2 hadi 4. Mie huwa napenda pilipili hoho zisiive sana, maana zinakuwa na virutubisho zaidi na harufu nzuri.
 • Mimina mchanganyiko wa yai kwenye kikaango. Acha lipate kuiva vizuri upande mmoja kisha geuze upande wa pili. Likiiva vizuri toa na hifadhi pembeni.
 • Kata nyanya na nusu karoti kwenye vipande vidogo, kama unavyopendelea kachumbari yako iwe.

2misosi

 • Pasua mkate katikati. Panga yai, na nyanya katikati ya mkate. Kama una sauce, mimina ili uweze kuongeza ladha.
 • Hiki ni chakula kamili, unaweza kunywa na kinywaji ukipendacho. Kinaenda vizuri pia na maji.
 • Jirambe na ladha ya maisha.

misosi-sandwich


MAPISHI YAPENDWAYO

Roast ya Samaki
dakika 30
Walaji: 3

Chips za kuoka zenye viungo
dakika 40
Walaji: 2

Wali wa bizari na viungo
dakika 25
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.