Sausage Stroganoff

Ukiwa umetoka kazini au mizungukoni na unataka kula chakula kitamu ambacho ni rahisi kuandaa, je ni chakula gani unafikiria? Pengine wengi wetu huwaza kuandaa tambi, kukaanga mayai au kupika sausage. Yote ni kheri, lakini inakuwaje kama unaweza kuleta vionjo zaidi kwenye chakula chako hata kama ni simple? Hapo ndio unapokutana na sausage stroganoff. Sausage stroganoff ni sausage zinazopikwa na maziwa. Kwa kawaida, nyama ya aina yeyote ikiwa na maziwa (mgando au maziwa fresh) huitwa stroganoff kwa kirusi :) . Stroganoff ni recipe ya Urusi (Russian recipe), lakini unaweza kuongeza vionjo vyako ili kuipa ladha zaidi.

Mahitaji

 • Sausage 4 (Binafsi nilitumia sausage kubwa za ng’ombe, nikatumia nusu tu kwa kukata vipande vidogo)
 • Mafuta ya kula (Nimetumia mafuta ya zaituni, olive oil)
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Pilipili hoho ½ , ikatwe vipande vidogo
 • Kitunguu 1, menya na kata vipande vidogo
 • Pilipili manga ½ kijiko kidogo
 • Maziwa mgando (sour cream) vijiko 4 vikubwa
 • Kitunguu saumu kijiko 1 kidogo
 • Nyanya (tumia nyanya zilizosagwa kwa matokeo mazuri)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Sausage stroganoff ni chakula rahisi kuandaa, lakini chenye utamu wa kukupa hamu ya kula. Unaweza kuandaa kwa kutumia viungo tofauti au ikawa rahisi. Kuwa huru kuongeza au kutoa kile unachoona hakikufai. Muhimu usiache kutumia maziwa, na ukikosa maziwa  ya mgando tumia maziwa fresh, matokeo huwa ni mazuri pia.

misosi-sausage-stroganoff-2

 • Bandika kikaango jikoni, weka mafuta ya kula kiasi tu ili kukaanga sausage. Acha yapate moto. Weka sausage na kanga vizuri, zisikae sana na kuungua. Toa na hifadhi pembeni na uzikate kwenye vipande vya wastani.

Mie huwa napenda kukaanga sausage kidogo kabla ya kuzipika kwenye sauce. Hii inafanya sausage ziwe na ladha nzuri zaidi na kuwa na mvuto wakati wa kula.

 • Bandika kikaango tofauti au sufuria jikoni. Weka mafuta, acha yapate moto. Weka kitunguu saumu, koroga. Weka kitunguu maji, koroga hadi kianze kubadilika rangi kiasi. Weka pilipili manga, koroga. Weka pilipili hoho, koroga kiasi. Acha kwa dakika 2 zichemke.
 • Weka nyanya, weka chumvi kiasi. Koroga vizuri. Acha zichemke na kuiva.
 • Weka sausage, koroga vizuri. Weka maziwa ya mgando, koroga kisha acha zichemke kwa dakika 2 hadi 3. Ni vizuri kuweka sausage mwisho ili zisiive na kuwa laini sana, zikiiva sana huwa hazina ladha kwenye kula. Pia unaweza usichanganye sausage kwenye sauce yenye maziwa bali ukamwagia sauce hiyo juu ya sausage wakati wa kula. Ingawa kwa mimi binafsi napenda kuchanganya wakati wa mapishi kwa ladha tamu zaidi.
 • Unaweza kula sausage hizi kwa wali, ugali hata tambi. Tenga chakula na jirambe.

misosi-sausage-stroganoff


MAPISHI YAPENDWAYO

Salad ya samaki
dakika 15
Walaji: 1

Mkate wa ndizi na mayai
dakika 75
Walaji: 16

Tambi na mayai
dakika 10
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.