Shawarma ya kuku

Shawarma ni chakula maarufu chenye asili ya nchi za mashariki ya kati. Jina la shawarma lina mizizi ya kituruki likimaanisha « kuzunguka », maana mara nyingi nyama yake huwa bonge kubwa la nyama ya kusaga ambalo huivishwa taratibu kwenye jiko kwa kuzunguka. Hii ni shawarma ya kienyeji, maana huna jiko la kuzunguka, hivyo unaweza kuandaa kirahisi kama maelezo yalivyo hapa.

Mahitaji

 • Minofu ya kuku gramu 200
 • Pilipili manga ya unga kijiko 1 kidogo
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Pilipili hoho 1
 • Kitunguu maji 1
 • Kitunguu saumu cha unga kijiko 1 kidogo
 • Karoti 1
 • Ndimu au limao ½ au unaweza kutumia vinegar
 • Curry powder kijiko 1 kikubwa
 • Mafuta ya kula, nimetumia mafuta ya zaituni (Olive oil)
 • Tortilla au chapati

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Chakula hiki ni rahisi na kizuri kula muda wowote, maana ni chakula chepesi kinachokupa afya bila kula sana. Nyama ya hii shawarma ilitengenezwa kama  maelezo ya hii nyama ya kuku hapa.

misosi-shawarma-main2

 • Andaa kuku – osha kisha kata vipande vidogo sana ili nyama iweze kuiva haraka na vizuri. Kamulia limao kisha changanya vizuri hadi nyama ienee limao. Nyunyuzia chumvi, koroa vizuri ili chumvi iingie kwenye nyama. Nyunyizia kitunguu saumu, koroga vizuri. Kisha hifadhi nyama pembeni.
 • Andaa pilipili hoho, kitunguu maji na karoti. Menya kisha kata vipande vidogo kwa karoti na kitunguu. Pilipili hoho kata vipande virefu na vipana. Vitapendeza zaidi kwenye shawarma.
 • Bandika kikaango jikoni, acha kipate moto sana. Weka mafuta kiasi. Acha hadi yapate moto. Weka nyama, tandaza vizuri. Acha iive kwa dakika 5 kisha geuza ili iive vizuri upande wa pili. Endelea kugeuza mara kwa mara ili nyama iive na maji yakauke. Nyama ikiianza kubadilika rangi, weka pilipili manga koroga vizuri. Baada ya dakika 2 toa nyama weka kwenye chombo safi pembeni.
 • Weka kikaango jikoni, kikipata moto weka mafuta ya kula kisha weka kitunguu maji. Kaanga vizuri hadi kianze kubadilika rangi. Weka pilipili hoho na karoti, koroga vizuri. Baada ya dakika 3 weka nyama ya kuku. Koroga pamoja vizuri. Vikichanganyika vizuri, weka curry powder. Koroga vizuri hadi curry powder iendee kwenye nyama na mboga za majani vizuri. Kisha epua weka pembeni.
 • Andaa tortilla au chapati, pamoja na sauce unazotumia kwenye kula shawarma kisha tenga vizuri chakula na ujirambe.

misosi-shawarma-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Nyama yenye curry sauce
dakika 25
Walaji: 6

Visheti vya vanilla na mdalasini
dakika 15
Walaji: 10

Chicken Tandoori
dakika 60
Walaji: 4

Shawarma ya kuku
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.