Shawarma za mayai, sausage, nyama na broccoli

Je una kiporo cha mboga kilichobaki na unahitaji kupata mlo mtamu wa kuchanganya? Basi hiki ndio chakula murua cha kuandaa. Chakula hiki kinakupa protini, nyuzinyuzi (fiber), wanga na mafuta. Ni chakula chepesi chenye mahsusi kuliwa usiku ili kutokula chakula kingi na kukuzuia kupata usingizi mzuri.

Mahitaji

 • Sausage 2
 • Mayai 2
 • Pilipili hoho 2 (Nyekundu na kijani)
 • Kitunguu 1
 • Karoti 1
 • Cub Maggie 1
 • Sandwich wrap (Chapati)
 • Tango 1
 • Nyama ya mchuzi iliyoungwa vizuri
 • Kabichi ya brokoli (Broccoli) vipande 2
 • Mafuta ya kula
 • Chumvi – kijiko cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Chakula hiki ni maalumu kwa kuliwa kwa viporo. Ni vizuri kama kuna mboga zilizobaki ili kula mlo mwepesi wenye virutubisho vinavyofaa. Hapa kwenye chakula kulikuwa na nyama ya kukaanga na asali, nyama ya kawaida ya mchuzi pamoja na viazi. Maelezo yanayotelewa hapa ni kuhusu kuandaa mayai yenye mchanganyiko wa mboga za majani na sausages.

 • Andaa vitunguu, pilipili hoho na karoti kwa kumenya na kukata kwenye vipande vidogo . Kata sausage kwenye vipande vidogo

Unaweza kukata vipande vikubwa au kuacha sausage bila kuzikata. Tatizo ni kuwa zitachelewa kuiva.

 • Weka kikaango jikoni, weka mafuta na subiria yapate moto.
 • Kwenye jiko tofauti, bandika sufuria, weka maji, kisha weka broccoli na chumvi ili ziive. Acha ichemke kwa muda kama dakika 10 hadi 15.
 • Weka kitunguu, subiria kiive vizuri kisha weka pilipili hoho na karoti. Koroga kiasi kwa muda wa dakika 1 hadi 2.
 • Pasua yai, weka chumvi na koroga hadi lichanganyike vizuri. Weka cube Maggie na koroga zaidi.
 • Mimina mchanganyiko wa yai kwenye kikaangio. Koroga na geuza hadi yai live.
 • Ipua na tenga chakula chako. Ni vizuri kama utapasha moto sandwich wrap ili kula ikiwa ya moto – ni vizuri zaidi.
 • Unaweza kuandaa kachumbari yako - mie hupendelea zaidi tango na nyanya. Unaweza kuamua utakavyo

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.