Spice potato curry

Mahitaji

 • Viazi ulaya kg 1
 • Bizari kijiko 1 cha chakula
 • Bizari nyembamba nusu kijiko cha chai
 • Mafuta vijiko 3 vya chai
 • Mbegu za mustard robo kijiko cha chai
 • Vitunguu maji 2
 • Nyanya 3 kubwa zilizoiva
 • Chumvi nusu kijiko cha chai
 • Kitunguu saumu cha unga nusu kijiko cha chai
 • Tangawizi nusu kijiko cha chai nimetumia ya unga
 • Garam masala kijiko 1 cha chakula

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Menya viazi, osha kisha kata umbo la mraba. Weka kwenye sufuria yenye maji, bandika jikoni na acha viive. Epua, chuja maji, hifadhi pembeni.
 • Bandika sufuria jikoni, weka mafuta ya kula. Mafuta yakipata moto, weka mbegu za mustard, kitunguu saumu, tangawizi, garam masala, na bizari nyembamba. Koroga kwa dakika 3 kisha weka vitunguu maji. Endelea kukoroga. Kaanga mpaka viwe rangi ya kahawia. Weka nyanya acha ziive mpaka zilainike, na mafuta yajitenge na nyanya. Weka bizari na chumvi, kisha weka maji kikombe kimoja na nusu. Funika acha ichemke.
 • Mchuzi ukianza kupungua, weka viazi. Changanya vizuri, kisha punguza moto.Pika kwa dakika 7 mpaka 10.
 • Mchuzi ukikaukia, epua chakula kisha jirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Vitumbua vya mayai
dakika 10
Walaji: 6

Brown rice, maziwa na karoti
dakika 60
Walaji: 1

Chicken Curry
dakika 30
Walaji: 3

Cornbread yenye korosho
dakika 40
Walaji: 6

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.