Spicy grilled prawns

Mahitaji

 • Prawns kilo 1
 • Pilipili manga vijiko 2 vya chakula
 • Kitunguu saumu 2
 • Tangawizi kijiko 2 iliyosagwa
 • Oyster sauce kikombe 1 cha kahawa
 • Olive oil kikombe 1 cha kahawa
 • Chumvi
 • Ndimu 1
 • Cayenne pepper kijiko 1 cha chai
 • Paprika kijiko 1 cha chai
 • Thyme kijiko 1 cha chakula
 • Mustard powder kijiko 1 cha chakula
 • Oregano kijiko 1 cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Chukua prawns, wasafishe vizuri. Wakamulie ndimu watie na chumvi. Waweke pembeni.
 • Chukua bakuli weka olive oil na viungo vyote. Changanya vizuri sana.
 • Chukua prawns, waweke kwenye ule mchanganyiko hakikisha wameendea viungo.
 • Hakikisha prawns wameenea viungo vizuri.
 • Funika bakuli vizuri au weka kwenye mfuko kisha waweke kwenye fridge. 
 • Acha wakae usiku mzima, au masaa 5. Chukua wavu wakuokea upake mafuta
 • Uweke jikoni ukipata moto panga prawns kua unawageuza baada ya dakikia 5, ukimgeuza unampaka ile sauce ya viungo.
 • Wakiiva jirambe na familia.

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.