Spicy Meatballs na mboga majani

Hizi meatballs zina utamu mzuri, wa kipekee na zinatia hamu ya kula. Uwepo wa pilipili umefanya hizi meatballs kuwa tamu na harufu nzuri. Ni mboga nzuri kula na vyakula aina tofauti. Jirambe na utamu wa hizi meatballs.

Mahitaji

Kwa ajili ya meatballs

 • Vijiko 2 vya mafuta ya zaituni (Olive oil)
 • Kitunguu maji 1, menya na kata vipande vidogo
 • Kitunguu saumu 1, menya na ponda
 • Kilo 1 ya nyama, kata vipande vyembamba na vidogo
 • Kijiko 1 cha rosemary
 • Yai 1, pasua na koroga
 • Chumvi kijiko 1
 • Pilipili manga ya unga kijiko 1

Kwa ajili ya sauce

 • VIjiko 3 vya mafuta ya zaituni
 • Kitunguu maji 1, kata vipande
 • Kitunguu saumu punje 5, ponda
 • Pilipili hoho 2, mie nimechanganya za rangi tofauti
 • Chumvi kijiko 1
 • Pilipili manga ya unga kijiko 1
 • Pilipili 2

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Hakikisha meatballs zinaandaliwa angalau masaa 12 kabla ya kupika na sauce. Usiandae na kupika moja kwa moja, haitokuwa na matokeo mazuri.

Kuandaa meatballs

 • Weka kikaango jikoni, acha kipate moto vizuri. Weka vijiko 2 vya mafuta ya zaituni kwenye moto wa wastani. Mafuta yakipata moto ongeza kitunguu maji na kitunguu saumu. Funika na acha vichuje maji kwa dakika 4 na viwe laini na rangi ya kahawia. Epua na acha vipoe.
 • Kwenye bakuli, changanya nyama iliyokatwa vipande vyembamba na vitunguu vya baridi. Ongeza viungo vingine na mayai. Weka chumvi na pilipili kulingana na unavyopendelea.
 • Gawa nyama kwenye mabonge 24, kulingana na ukubwa unaopenda. Weka meatballs kwenye mfuko au chombo cha kuhifadhia kwenye jokofu. Hifadhi kwenye jokofu ili zigande hadi pale unapohitaji kuzitumia.
 • Ukihitaji kupika, toa meatballs, hifadhi pembeni. Bandika sufuria au kikaango jikoni kwenye moto mkali, weka mafuta ya kula, acha yapate moto vizuri kisha weka meatballs. Acha meatballs hadi ziive kisha toa na hifadhi pembeni. Hifadhi kwenye karatasi au tissue ili zichuje mafuta.

Kuandaa sauce

Kwenye mboga hii unaweza kuongeza viungo unavyopendelea ili kupata mboga bora na tamu.

 • Osha kisha kata pilipili hoho, kitunguu saumu, kitunguu maji na pilipili za kawaida. Hifadhi kwenye chombo safi pembeni.
 • Bandika kikaango au sufuria jikoni. Kikipata moto weka mafuta ya kula vijiko 2, acha yapate moto vizuri kisha weka kitunguu maji na kitunguu saumu. Funika ili vipate kulainika na kuchuja maji ili wive laini na kuwa rangi ya kahawia.
 • Weka pilipili hoho, koroga kiasi. Weka pilipili za kawaida, koroga zaidi. Funika sufuria vizuri, acha vichemke pamoja kwa dakika 5.
 • Weka meatballs, koroga vizuri. Acha vichemka pamoja kwa dakika 5 hadi 7. Epua na kisha andaa pamoja na wali, ugali au pasta.

spicy-meatballs-misosi-poor


MAPISHI YAPENDWAYO

Meatballs za viungo
dakika 30
Walaji: 4

Viazi na meatballs za nazi
dakika 20
Walaji: 4

Tambi za mayai
dakika 15
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.